Wizara ya Fedha ya Tanzania Iboreshe Elimu ya Kodi

MasterGamaliel

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
813
874
Nani hubeba mzigo wa Kodi?

Miaka michache iliyopita iliwahi tokea bank withdrawal charges zikaongezwa Kwa order ya serikali ikiwa ni kwamba ile nyongeza iwe pesa ya serikali Kwa hoja kwamba bankers (mtoa huduma) ndiye anayepaswa kulipa ongezeko la bank charges hizo.
Hali ile iliwafanya wataalamu wa maswala ya 'Kodi ya Ulaji bidhaa/huduma' watolee ufafanuzi kuhusu Nani huumizwa na kifinyo cha Kodi!

Ikaeleweka kuwa mtumiaji (mlaji) wa hudumu za bank ndiye atakayelipa, na ikawa hivyo hadi Leo.

Hivyo hivyo inapaswa ieleweke (ikumbukwe) kuwa hata Kodi kwenye rent ya nyumba hii inayoanza kuwa exercised soon, atakayelipa (atakayefinyika) ni mpangaji aliyekubali kula huduma ya pango la mpangishaji.

Utayari na uwezo wa mlaji bidhaa au huduma ndio chanzo halisi cha Kodi.

Atakayempa uwezo wakala wa tozo/Kodi ni aliyeweza kupanga tu.

Kinachoumiza Sana wananchi kuhusu Kodi ni uwepo wa wanufaika wa hizo Kodi kifisadi, ama kibinafsi (ukwapuaji), upendeleo wa miradi kikanda au wa ajira Kwa watoto wa wanaodhani wazazi walitumikia nchi kuliko watoto wa wazee wengine, udini, ukanda, na UCCM na mengine mengi.

Niishie hapo lakini upeo wenu uwe pamoja nanyi.

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom