Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Kuna wakati unaweza hisi labda unaangalia maigizo au ze comedy ukiwasikiliza viongozi wetu. Mfano, siku ya mei mosi nilimsikia waziri mmoja akimwambia Rais kuwa yuko tayari kutumwa!? siku ile nilijiuliza, hivi mawaziri hawanaga job descriptions hadi amuombe Rais amtume!? kwani aliteuliwa ili iweje!? je, hajui majukumu yake!? Nikaishia hapo ili nisije nikajiumiza kichwa kwa mambo ya hawa wakubwa.
Siku nyingine nikamskia Rais anasema kuwa hataki kuona wafanyabiashara wa sukari wakiagiza sukari kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani! Tena hakuishia hapo, akasema na bei ishuke hadi TSH.18,000/= kwa kilo moja. Nilijawa namatumaini kwa sababu huko nyuma nilishaambiwa kuwa kauli ya mkubwa ni kama sheria! Nikafurahi kweli kweli kwamba angalau nitaanza kuweka japo akiba itakayopungua kwa kila kilo ya sukari nitakayo nunua. kilichotokea baada ya hapo hadi leo sijaelewa! Naishia kuilaumu TV yangu iliyonionyesha jambo ambalo huenda yule mtangazaji alipitiwa. Baada msaidizi wake mkuu akatwambia basi itakuja hadi 2,200/=, mwingine naye akasema itakuuzwa hadi 2,500/=
Siku nyingine tena nikamskia anawaambia wakuu aliokuwa amewateua kuwa kipimo chao cha kwanza ni kwenda kuondoa vivuli vilivyokuwa vinalipwa mshahara na kuhakikisha kila mtoto wa masikini anakaa juu ya dawati. Pa kupata vitendea kazi watajua wenyewe wala wasimuulize tena akawapangia na muda. Sijui kama wameshamaliza.
Sasa leo kuna hii kitu VAT! ...a tax that is added to the price of goods or services(simple definition from Advanced learners dictionary) yaani kama bei ya huduma au bidhaa ilikuwa 2500, inapoletwa VAT kwenye hiyo huduma bei itabadilika na kuwa 2500+VAT. Sasa juzi benki mbalimbali zilianza kuwaarifu wateja wao kuwa zitaanza kuisaidia serikali(kwa sababu ndio jukumu lao)kukusanya hiyo VAT kwetu! TRA wanakuja juu kwamba sio sahihi wanachotaka kufanya. Wanamuomba Gavana aingilie kati yeye anawajibu rahisi tu kuwa mabenki yako sahihi kwa mujibu wa sheria za utozaji wa hiyo kodi. Ni kodi inayolipwa na mtumiaji wa mwisho.
Hivi wakati wabunge wanapitia hii bajeti, hili hawakulijua!? Je, ni kweli kuwa TRA na wizara ya fedha hawakujua hii kodi atakayeilipa ni nani!? Wako makini kweli kutwambia kwa staili hii tutafikia nchi ya viwanda!? DIRA BILA MATENDO NI NDOTO ZA MCHANA. Kuna wakati wa siasa na wakati wakulitumikia Taifa kwa uaminifu.