Wizara ya Fedha kununua Laptop 220, printer 110, photocopier 9 , TV 40, Fax 13 kwa ajili ya Mkutano

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,873
4,273
Kwa mujibu wa tangazo lililotoka kwenye kwenye gazeti la leo la the Guardian la leo, Wizara ya fedha imetenga fedha kwa ajili ya kununua laptop 220, printers 110, photocopier 9 TV flat screen 40 photocopier 9 na fax 13, server 1 n.k kwa ajili ya mkutano wa mwaka wa African development Bank. Swali langu ni je ni kweli mkutano wa siku 3 unahitaji investment kubwa naona hii? Naamini wajumbe wote wa mkutano wana laptops zao, hawawezi kuambiwa kila mshiriki aje na laptop kama ni lazima huo mkutano unahitaji washiriki kuwa na Laptops? Halikadhalika waandaaji ambao ni maafisa nao wana computer zao, je hawawezi kutumia vifaa vyao walivyonavyo katika kuandaa mkutano huu.
 
Kama kweli wanahitaji hivyo vifaa vyote kwa mkutano wa siku 3 ni bora wangeazima mahali then mkutano ukiisha wanarudisha..
 
Kila mtu atakula mezani kwake, na /au kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba aliyofungiwa, na basi wanunue hivyo vifaa wafaidi. Na inawezekana hata huko kutangaza ni gheresha kuridhisha tu kumbe vifaa vimeshanunuliwa zamani, Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!
 
ole wao wanaoifaidi keki ya taifa bila kuwafikiria wenzao,mwisho wao utafika na utakuwa ni mwisho wa aibu kubwa sana kwao na kwa jamaa zao.
:embarassed2:
 
kwa mujibu wa tangazo lililotoka kwenye kwenye gazeti la leo la the guardian la leo, wizara ya fedha imetenga fedha kwa ajili ya kununua laptop 220, printers 110, photocopier 9 tv flat screen 40 photocopier 9 na fax 13, server 1 n.k kwa ajili ya mkutano wa mwaka wa african development bank. Swali langu ni je ni kweli mkutano wa siku 3 unahitaji investment kubwa naona hii? Naamini wajumbe wote wa mkutano wana laptops zao, hawawezi kuambiwa kila mshiriki aje na laptop kama ni lazima huo mkutano unahitaji washiriki kuwa na laptops? Halikadhalika waandaaji ambao ni maafisa nao wana computer zao, je hawawezi kutumia vifaa vyao walivyonavyo katika kuandaa mkutano huu.

kamalizie kusoma vizuri tangazo! hiring ni kununua?
 
Nahisi kitakachofuata hapo ni kwa maofisa hao wa serikali kuuziana hizo laptops kwa elfu kumi kumi tu baada ya mkutano kuisha maana yake watasema hazina kazi tena. Printa wanaweza kugawana hata bure kwa vile zitakuwa mitumba tayari. Hiyo ndo nchi yetu masikini inayokaribia kuongoza duniani kwa kuomba misaada kutoka kwa hao wanaoitwa wahisani. Kidogo tulichonacho hatujui hata namna ya kukitumia. Kazi tunayo!
 
Aliposema jk serikali haina pesa nlijaribu kumpa benefit of doubt japo kidogo lakini kwa hili inatia mashaka.. mbona haya matumizi yanaonekana kabisa hayana tija na haihtaji uwe na elimu kubwa ili kujua hili..

NAWASI WASI MKUBWA NA UWEZO WA WATENDAJI WA SAFU YA JUU WA WIZARA YA FEDHA. NADHANI KUNAHAJA YA SERIKALI KUWATAZAMA UPYA.
 
habari za ufisadi zitakoma lini Tanzania?
hihi suala la mkurugenzi wa TBS limeishia wapi?
natamani kujifunga bomu niwamalize mafisadi wote wanakera sana,watu tunakufaa njaa wagonjwa hawana vitanda,madaktari wamegoma
sasa wanaendekeza upumbafu namna hiii? hata nchi tajiri hawafanyi upuuzi huu na hata vikao hawana allowance sisi maskini eti laptop??? haingii akili bora wasee wananunua files wawagawie sio laptop,kweli tunaongozwa na watu vilaza na wasiokuwa na uchungu na nchi yao,hata aibu hawana??shame on them
 
Nchi inaliwa kila siku, ukisoma gazeti la East African la leo (Feb.6-12) utachoka mwenyewe. Jamaa wamekomba $ 54 m kwenye mafuta ya IPTL.
 
Fedha zinazotokana na Rasilimali kama Madini ndizo zinazotumika kununua thamani za Ofisini badala ya kuwekeza katika viwanda na teknolojia nyingine.
 
Kwa mujibu wa tangazo lililotoka kwenye kwenye gazeti la leo la the Guardian la leo, Wizara ya fedha imetenga fedha kwa ajili ya kununua laptop 220, printers 110, photocopier 9 TV flat screen 40 photocopier 9 na fax 13, server 1 n.k kwa ajili ya mkutano wa mwaka wa African development Bank. Swali langu ni je ni kweli mkutano wa siku 3 unahitaji investment kubwa naona hii? Naamini wajumbe wote wa mkutano wana laptops zao, hawawezi kuambiwa kila mshiriki aje na laptop kama ni lazima huo mkutano unahitaji washiriki kuwa na Laptops? Halikadhalika waandaaji ambao ni maafisa nao wana computer zao, je hawawezi kutumia vifaa vyao walivyonavyo katika kuandaa mkutano huu.

Kwa nini tusiamini Africani development bank wametoa fedha zao kwa tanzania ktk maandalizi ya mkutano huo lakini tukaamini tu kwamba sisi ndo tunanunua? nani anyejua mkutano kama huo kwa mara ya mwisho ulifanyika wapi? na wenzetu waliundaa vipi? aweze kutujuza ili tuchukue hiyo kama benchmark yetu
 
Fedha kwa ajili ya matumizi ya kipuuzi zipo,ila fedha ya matumizi ya maendeleo ya wananchi na maeneo mengine nyeti kama afya hakuna. Kama serikali haina fedha mbona hivyo viwanda vinavyotembea"mashangingi" hayaja simama "parked"
 
Kwa mujibu wa tangazo lililotoka kwenye kwenye gazeti la leo la the Guardian la leo, Wizara ya fedha imetenga fedha kwa ajili ya kununua laptop 220, printers 110, photocopier 9 TV flat screen 40 photocopier 9 na fax 13, server 1 n.k kwa ajili ya mkutano wa mwaka wa African development Bank. Swali langu ni je ni kweli mkutano wa siku 3 unahitaji investment kubwa naona hii? Naamini wajumbe wote wa mkutano wana laptops zao, hawawezi kuambiwa kila mshiriki aje na laptop kama ni lazima huo mkutano unahitaji washiriki kuwa na Laptops? Halikadhalika waandaaji ambao ni maafisa nao wana computer zao, je hawawezi kutumia vifaa vyao walivyonavyo katika kuandaa mkutano huu.
tunafaidika nini na huu mkutano au ni yale ya SULVAN kule Arusha?? baada ya mkutano computer zinabaki au wajumbe wanasepa nazo??
 
Back
Top Bottom