Wizara ya Elimu yasema tathmini waliyofanya imebaini ni ngumu kuongeza saa 2 za masomo, Shule zaelekezwa kufuata ratiba za masomo 8 kama zamani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wizara ya Elimu imetolea ufafanuzi ongezeko la saa 2 za masomo kwa Wanafunzi baada ya Shule zote nchini kufunguliwa ili kufidia muda ambao umepotea kutokana na mlipuko wa CoronaVirus

Wizara hiyo imesema tathmini waliyofanya imebaini jambo hilo ni gumu kutekelezeka kwasababu kuna Shule zenye vibali vya kuendesha masomo kwa mfumo wa 'double shift'. Pia suala la usafiri kwa wanafunzi waishio mbali nalo limeonekana kuwa ni changamoto

Kutokana na hilo, Wizara imezitaka Shule kutumia ratiba za vipindi 8 kama ilivyokuwa awali na Shule zitakazoona umuhimu wa kuongeza muda wa masomo zitatumia muda uliopangwa kwenye ratiba zao
 

Attachments

  • KUREKEBISHA.pdf
    119.7 KB · Views: 28
QUOTE="Tate Mkuu, post: 35888494, member: 535381"]
Kwa hiyo Mheshimiwa alikurupuka kutoa tamko lisilo tekelezeka! Hatari sana. Kuna umuhimu sasa wa kuachana na haya mambo ya One Man Show!!
[/QUOTE]
Bunge lilipo vunjwa alisema siku hiyo halali hadi ratiba zoote zipangwe upya. Sasa nilitegemea tuu. Kwenye idara ya elimu na wizara yake yaan kuna kitabia cha kukurupuka na kutumia common sense na kuacha kufuata sheria kanuni na taratibu zilizowekwa. Na mbaya zaidi waalim wanaongozwa na matamko na hisia za wakuu wao ni shidaaaaa
 
walimu walio nitukana mimi enzi na enzi njooni tena muitukane wizara.
mm enzi na enzi nilisema ulikuwa mpango wakulisha familia za walimu nikaishia kubezwa.

selikari sikivu.
hayo nimajibu ya juhudi zangu kuwapigania wananchi wanyonge

by Enzi na Enzi.
 
Back
Top Bottom