benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,032
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam kueleza mikakati ya wizara yake ambayo ikiwemo utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/23 iliyopitishwa bungeni amesema Serikali imetenga shilingi Bilioni 3 kwa mwaka huu kwa ajili ya kuwezesha ufadhili kwa wanafunzi ambao wamepata ufaulu mkubwa katika elimu ya juu kupitia masomo ya sayansi
“Kigezo cha atakayepatiwa ufadhili huo ambao wengi wanataka uitwe Samia Scholar ni kufaulu vizuri katika masomo ya sayansi na upo tayari kuendelea na kusoma masomo ya uhandisi,elimu tiba.Kwa sasa tunatoa udhamini huo kwa vyuo vya ndani tu,”amesema Prof.Mkenda.
Amesema wataweka dirisha kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili nao waweze kunufaika na ufadhili huo ambao utakuwa unatolewa bila kujali huyu katoka wapi au familia gani, ilimradi awe amefaulu vizuri sayansi na afahamu kuwa, anasoma kwa kodi ya Watanzania, hivyo anapaswa kuonesha bidii ili aje kuwahudumia kupitia taaluma yake.