Wizara ya Elimu ya Juu irudishwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Elimu ya Juu irudishwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masaki, Oct 24, 2008.

 1. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kwa kipindi kirefu sasa tumekuwa tukisoma kwenye vyombo vya habari juu ya migomo na maandamano ya wanafunzi na walimu kuanzia ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu. Wanafunzi wana matatizo makubwa kuanzia ukosefu wa vyoo, madawati, chakula, maabara, malazi na huduma nyingine muhimu. Walimu nao hawajalipwa mafao yao na mishahara yao kwa kipindi kirefu kiasi cha kuonekana kwenye vyombo vya habari wakiwa wanalia machozi hadharani!

  Wakati Rais anapangua Baraza lake la Mawaziri na kuunda jipya, watu wengi tulifurahia kwamba alipunguza ukubwa wa Baraza hilo. Lakini katika vitu vilivyonitia shaka sana ni kitendo cha kuunganisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na ile ya Elimu ya Juu.

  Ifahamike kwamba, moja kati ya sekta zenye matatizo mengi sana katika nchi yetu ni Elimu. Wakati Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwa peke yake na ile ya Elimu ya Juu pia ikiwa peke yake, bado kulikuwa na matatizo lukuki ya kutatua.

  Leo hii mzigo wote umerundikwa kwenye mabega ya Waziri mmoja ambaye sasa ni dhahiri kabisa kwamba ameelemewa!

  Napendekeza Wizara hizi mbili zirudishwe kama ilivyokuwa mwanzo ili kuongeza ufanisi na tija katika utendaji. Elimu ndio mhimili wa maendeleo ya taifa hili na sio kitu cha kufanyia mzaha mzaha tu!!!

  Naomba kuwakilisha!!!
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna haja ya kuirudisha ni kuongeza mzigo tu kwa serikali wizara moja inatosha kabisa
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Kwani waziri ndo mtendaji? ninachofahamu mimi hakuna watendaji waliopunguzwa baada ya kuunganisha wizara hizo. endapo itadhihirika kuwa utendaji wa wizara unashuka kwa sababu waziri anamajukumu makubwa basi tumekwisha.

  Wizara ya elimu kuna Katibu Mkuu, naibu katibu Mkuu, wakurugenzi (elimu ya Msingi, Sekondari, elimu ya watu wazima,elimu ya juu) pia kuna idara ...

  Mtazamo wangu ni kuzidi kupunguza Wizara ili wanasiasa wawe wachache katika ngazi za utendaji. Wanasiasa ndiyo wanaosababisha matatizo ya ovyo kama Richmond, IPTL etc. watendaji wasipoingiliwa wanaweza kufanya kazi nzuri sana.

  Hivyo Mkuu, ninapingana na wewe kabisa kimsimamo. Ningefurahi endapo tungekuwa na mawaziri 10 - 15 tu.
   
 4. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  There is no need for that, waziri hawezi kuzuia matatizo yaliyopo unless serikali itoe resources zaidi na watu wapewe haki zao kama zinavyotakiwa.
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pole sana ndugu yangu Masaki!!!

  Tatizo kwani ni wizara?? Kama ungejua historia ya wizara hiyo Tangu iko chini akina Ben Mkapa na Bilal basi hungepoteza muda wako kuililia.

  Hapa tatizo si wizara bali ni kushindwa kwa mfumo mzima wa utawala (governing system). Sidhani kama unaweza kunipa mfano wa wizara yoyote katika nchi hii imbayo imeweza kutekeleza majukumu yake angalau kwa 50%! Ukipata mfano huo basi ulete hapa tuanze mjadala upya.

  Kwa hiyo kazi tuliyonayo ni moja tu. Kufumua mfumo mzima wa kiuongozi na utawala wa nchi hii (total revamption) ili tuanze moja; kwa kuweka vipau mbele upya (setting priorities) na mikakati mipya (road map) ambayo imekubalika na wadau wote. Hapa hakuna chama wala mtu wa kushika hatamu, it's National concensus. Baada ya hapo tuanze kwenda mbele. Kwa hiyo jukumu langu na lako ni kufanya ukombozi mpya wa taifa letu kwa kuondoa watawala hawa wasio na malengo yoyote ya maana kwetu (mission and vision) badala yake wanafanya usanii na maisha yetu!
   
 6. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Bwana Masaki,
  Mimi nadhani tatizo sio idadi ya wizara kuwa chache, ila ni wizara kuwa nyingi, matokeo yake maamuzi ya wanasiasa yanaingilia zaidi utendaji wa kitaalamu katika sector nyingi.

  Ukibahatika kuzungumza na watendaji wa wizara mbali mbali, watakuwambia hawajui nini ni kazi za mawaziri na manaibu waziri kiasi cha wizara nyingine kuwa na hawa watu 3 (waziri 1?manaibu 2). Mimi nadhani tatizo ni mfumo wa utawala, na ndio sababu sehemu nyingi zimekwama.

  Si ndio sababu unaona kila kitu anasubiriwa rais atoe kauli! wewe huoni hii shida? Isingekuwa hivyo sakata nyingi nchini zimekuwa zimekwisha kwani richmond, epa, meremeta, ubinafsishaji usiozingatia sheria n.k yangekuwa tayari yalishaisha, lakini tatizo ni uchache wa wizara au mfumo?
   
Loading...