Abuwhythum
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 837
- 495
Hivi bado mnahakiki tu vyeti vya walimu wa Sayansi na Hisabati!? Mbona majina mnayo toka vyuoni.
Kuweni wawazi kama mlivyokuwa wawazi kwa walimu wa sanaa! Waliumia sana lakini mtu amepewa ukweli na anajipanga na jambo la kufanya, hata walimu tarajali wa Sayansi na Hisabati waambieni ukweli kuwa ajira ni mwezi fulani, hata kama ni hadi mwaka ujao wa fedha semeni tu! Maana fursa nyingi zimepita kwa walimu hawa kuishi kwa dhana kuwa ajira huenda ni mwezi huu, mara unapita kimya, basi mwezi huu nao unaondoka kimyaaa! Basi huu nao huoooo kimyaa.
Kauli yenu ndogo tu yenye uwazi itaondoa malalamiko haya ambayo hayaishi kila siku.
Ukweli na Uwazi ni suala moja muhimu sana tena sana.