Wizara ya Elimu toeni mwongozo kuhusu likizo za wanafunzi

iddhassan

Senior Member
Jul 26, 2016
100
133
umezuka.mtindo baadhi ya shule za binafsi kwenda kinyume na mwongozo wa Wizara kwamba wakati wa likizo watoto wabaki shuleni kujisomea halafu walipie.

Mbaya zaidi siyo yale madarasa ya mitihani yaani form 2 na 4. Hivi serikani inapopanga muda wa kosoma kwani kwani hawana lengo?

Kwanini mjipangie utaratibu wenu wakati wizara ipo?.kwa nini mchukue pesa za wanyonge kwa kisingizio dhaifu kujiandaa zaidi?

Serikali inapopanga muda kwani hawana akili?mbona kama mna uchungu na elimu ya watoto isiwe bure?

Unamwambiaje mzazi alipe ada juu ya ada eti kubaki shuleni kujiandaa zaidi. Hivi watoto ni mashine hawahitaji kupumzika?

Tunaomba sana Serikali yetu sikivu itoe mwongozo muda halisi wa watoto kusoma siyo kuwaachia wenye shule binafsi kujiamulia wanavyopenda kwa.maslahi binafsi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom