Wizara ya Elimu Tanzania

Kapo Jr

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
996
280
Wizara ya elimu ni wizara nyeti inayogusa maisha ya wananchi karibuni wote,kinachoshangaza imegeuzwa kama kijiwe kwani tangu 2005/06 mitaala imebadilishwa kiholela kiasi ambacho kinazidi poromosha kiwango cha elimu na kupunguza soko la ajira,tukifumbia macho hili tutajutia chukulia mfano siku hizi kuhitimu elimu ya msingi(darasa la saba)hisabati mtihani wake majibu ya kuchagua tena kwa penseli na ufuto maalumu,wapi inaelekea elemu nchi hii?
 
Bodi ya mikopo kilio kwa waendao chuoni kuna chembe ya upendeleo jambo linaloleta chuki miongoni mwa wananchi,hili ni tatizo pia
 
Bila kufanyiwa mabadiliko yenye tija ni hatari mbele yetu
 
Mkuu tulishakosea tokea 2005 wakati wa kupiga kura halafu ukarudia tena kosa 2010 kwa kupewa tshirt na pilau sasa kwahiyo vumilia mpaka 2015 usirudie tena !!!!!!!!!!!!!!
 
Hata wao hawajui maana ya elimu,
Kwa kuwa hata watoto wao wanapata div.iv
wanarizika na wanawapeleka form v.
 
Tanzania kila watu wanafanya kazi kwa mazoea na wanavyotaka na kwa kweli wizara hii ndio inaweza kuongoza maana inaonekana kama hawajui wajibu wao na hasa kushughulikia kero za walimu na mambo ya msingi katika kuboresha elimu nchini nafikiri wamekosa mtu shupavu wa kuwasimamia.
 
Kwa kweli wizara hii ingefumuliwa na kuundwa upya kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo
 
Jamani naomkba kuuliza!
:israel:Inakuwaje kiongozi mmoja anakuwa na vyeo kibao!! Mkuu wa mkoa, mbunge, m/kiti wa bodi, mwekahazina!
 
Kiongozi msikivu,angetatua mapema kwa kuwateua watu waliobobea katika taaluma ili kunusuru anguko kuu kielimu
 
Muundo uliopo haufai kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu nchi,mfano kumekua na lawama kwenye bodi ya mikopo na hata baraza la mitihani ,utendaji wao wa mashaka
 
Back
Top Bottom