MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,006
- 2,166
Baada ya ajali na kupoteza maisha ya watoto kule Kagera, shule nyingine mkoani Tabora imeungua. Mmoja katika waliohojiwa alionesha mashaka kwamba kwa nini kwa muda mfupi kiasi hiki na kwa nini zote za dini moja - alimaanisha za Kiislamu.
Binafsi nina tatizo na ubora na tabia ya kupeleka watoto wa primary shule za boarding. Hakuna sababu ya kumpeleka mtoto wa primary boarding maana hata walio yatima wanalelewa sehemu maalumu pia na siyo shuleni.
Umri wa miaka 6 hadi 13 ni umri wa kujifunza lugha mbalimbali na ni umri wa kupata tabia na ulinzi maalumu kutoka kwa wazazi. Vyote hivi hutavipata shuleni. Inapotokea ajali kama hiyo ya moto, hawa ni watoto wasioweza kujiokoa. Ni watoto ambao hata maisha ya kawaida, hata kuamka ni kitendo wanachohitaji msaada! Je, nani awaokoe kwa wingi wao?
Shule zimejengwa kama kambi za kutwa! Hazina miundombinu ya kuzima moto, hata maji ya kuoga ni kubahatisha tu! Kwa ujumla ni shule za mtaji mdogo wakati watoto wanahitaji makubwa zaidi ya hayo. Hakuna walezi waliosomea kulea watoto.
Tuachane na mikogo ya boarding kwa watoto wadogo kiasi hiki. Kama ni kiingereza watakifahamu tu kwa day schools.