Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeruhusu wanafunzi wenye akili kurushwa madarasa?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,304
12,965
Kuna mwanafunzi nimesikia akitangazwa na kuhojiwa Clouds FM katika kipindi cha Power Breakfast kuwa amesoma elimu ya sekondari miaka miwili tu na kuhitimu badala ya miaka 7 ya kawaida. Maelezo yaliyotolewa ni kuwa alikonekana ana akili sana akarushwa kutoka darasa la kwanza hadi la nne. Baada ya hapo akafanya vizuri mtihani wa darasa la nne akarushwa hadi la saba na sasa hivi yuko Pre form one akijiandaa kwaajili ya kuingia kidato cha kwanza mwakani 2018

Swali langu ni kuwa utaratibu huu unarushusiwa kwa mujibu wa sera na kanuni za elimu kuwa mtoto mwenye akili anaweza asisome baadhi ya madarasa na badala yake akasoma madarasa yenye mitihani ya taifa tu. Inavyoelekea mtoto huyo kwa utaratibu waliojipangia hao wanaomrusha si dhani kama wanamsaidia mtoto huyo kupata maarifa yaliyokusudiwa kwani kusoma siyo kufaulu mitihani tu ni pamoja na kupata maarifa na elimu husika. Mwaka huu baadhi ya wanafunzi waliojiunga na shule za sekondari za binafsi kabla ya kumaliza darasa la saba walilazimika kurudi shule za msingi kumalizia elimu ya msingi baada ya serikali kubadili utaratibu wa usajili wa wanafunzi kwaajili ya mtihani wa kidato cha pili ambapo watasajiliwa iwapo watakuwa wamemaliza darasa la saba na kuwa na namba ya mtihani huo. Hivyo kutokana na sababu hiyo ikabidi warudi kumaliza darasa la saba ili wasikose usajili wa kidato cha pili ambao ndio pia mtihani wake huwa ni sifa ya kumsajili mwanafunzi kwaajili ya mtihani wa kidato cha nne.

Kwa upande wa elimu ya msingi ni kuwa mwanafunzi anasajiliwa kufanya mtihani wa darasa la nne akiwa amefanya mtihani wa darasa la pili. Na darasa la saba mwanafunzi anasajiliwa kufanya mtihani hauo baada ya kufanya mtihani wa darasa la nne na lazima miaka inayotofautisha mitihani hiyo izingatiwe kwa maana ya kwamba mwanafunzi hawezi akafanya mtiahani wa taifa wa darasa la nne mwaka jana halafu asajiliwe kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu 2018 kwani huyo ni wa kufanya mwaka 2020 Sasa kwa suala la huyo mwanafunzi anayedaiwa ana akili sana hivyo kuvushwa madarasa kwa mtindo ulioelezwa ina ruhusiwa? Na kama inaruhusiwa je ni utaratibu gani unatakiwa kufuatwa?
 
Mwanafunzi kuwa na akili mnatumia vigezo gani kum classify. Ninachojua mwanafunzi anajiweza darasani na si kwamba ana akili.

Ni maoni yangu.
 
Back
Top Bottom