Wizara ya Elimu: Rudesheni utaratibu wa kuwapima ujauzito watoto wa kike mashuleni

Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
403
677
Mheshiwa Magufuli nimekuelewa! "Shule za msingi na sekondari, si shule za wazazi"

Hii itasaidia kuwafanya watoto wetu wa kike kutafakari kabla ya kujiingiza na kujihusisha na mahusiano yatakayopelekea kupata ujauzito.


Mheshimiwa Rais, sisi ambao tumekuwa na umri mkubwa kidogo kuelekea utu uzima sasa, tunakumbuka sana katika shule zetu za wakati huo, zote msingi na sekondari, kulikuwa na utaratibu wa kila mwezi ambapo watoto wakike walipelekwa kufanyiwa vipimo vya ujauzito.

Naona kama utaratibu huu umepuuzwa, au hautiliwi maanani! Hebu sasa mkumbushe waziri wako wa elimu arudishe huo utaratibu. Hii itasaidia kudhibiti mimba mashuleni.

Wanajamvi, ninawasilisha hoja.
 
Kuwapima Mimba kutasaidia kuwajua wenye Mimba,hakusaidii kupunguza Mimba mashuleni
 
Kuwapima Mimba kutasaidia kuwajua wenye Mimba,hakusaidii kupunguza Mimba mashuleni

Haswaa! Wakimdaka tu hapo, fukuza akajifungue nyumbani! Na itakuwa imeepusha kishawishi cha kitoa mimba. Maana wataiona ikiwa changa kabla washauri wa kutoa hawajamfikia. Mtoto pia atakuwa ameokolewa.[
 
52615d6265f4b2195b7e089621dc0bf7.jpg

Hii ni ilani inayoongoza na iliyopigiwa kura na watanzania
 
Back
Top Bottom