Wizara ya elimu na utamaduni na.adhabu dhidi ya wandanganyifu wa mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya elimu na utamaduni na.adhabu dhidi ya wandanganyifu wa mitihani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hhm, Feb 16, 2012.

 1. H

  Hhm Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wana Jamii na watanzania kwa ujumla nimesikiliza hotuba mbalimbali za viongozi wa wizara ya elimu waliopewa dhamana. Hotuba walizotoa kimsingi sioni kama zina tija kwa twigs letu juu ya udhibiti wa udanganyifu wa mitihani..ninasema hivi nikimaanisha kuwa, adhabu iliyotajwa yakumfungia mtoto aliyedanganya katika mitihani MILELE kama ilivyokuwa ikisisitizwa kwa mtazamo wangu nikuongeza idadi ya wajinga nchini...Tuanze na system ya elimu nchini ilivyo tuiangalie na tuijadili kuona kama kweli inamuandaa mwanafunzi kufanya vyema akifika kidato cha nne na sita....pili tuangalie hao Waalimu waliopewa dhamana yakuelimisha Serekali inawajibika kwao kikamilifu?, tatu mazingira yaliyopo yanampa mwanafunzi fursa ya kusoma vizuri?? Mimi kwa mtazamo wangu System mzima ya elimu Tanzania iangaliwe upya mwafunzi achujwe mpaka anapofikia kidato cha nne tupate Wanafunzi bora ambapo hakika watafanya vizuri, mitihani ya form two inhehamishiwa form three ili mwanafunzi achujwe pale na akifeli arudie siyo kumfukuza.... Pamoja na hayo walimu wapewe mishahara mizuri na kuwepo na utaratibu wa kuwapa Waalimu motivation wanapofanya vizuri...mwanafunzi anapofanya udanganyifu afunguliwe mashtaka mahakamani na kuwepo na adhabu itakayomfanya mwanafunzi asithubutu kuiba mtihani.
   
Loading...