Wizara ya Elimu na Mh.Raisi Jpm hili mmeribariki au tunaibiwa?

okiwira

JF-Expert Member
Jul 23, 2018
2,787
2,853
Swala hili lipo Mbeya Rungwe Kiwira kata ya Ikuti katika shule ya msingi ikuti.

Wazazi wote ambao watoto wao wameingia darasa la kwanza mwaka huu ni lazima wapeleke tsh15000 la sivyo watoto wao watarudishwa chekechea.

Mwalimu mkuu na waliounda utaratibu huu mpya kwa walio wengi wanadai pesa hiyo ni kwa ajili ya cheti cha kuzaliwa.

Wanadai vile walivyopewa bure mahospitalini ni kwa ajili ya watoto wenye chini ya miaka mitano.

JE MH.RAISI JPM NA WIZARA HUSIKA MMEBARIKI KAZI AU TUNAIBIWA?
 
Hapo mnaigwa mkuu, hakuna utartibu kama huo uliopangwa na serikali.
Halmashauri ya Rungwe wana mambo ya ajabu ajabu kweli aisee.
Kuanzia kwa wakuu wa Idara wengi wao wamekaa kirushwa rushwa tu.
Hata hilo lazima kuna mtu nyuma ya pazia.
 
Kama ni kupigwa basi haizidi 5000 (kama ni kweli)

Huku kwetu ni 10000 ila unailipia bank
 
Wakuu tulienda wilayani Tukuyu wakatuambia vyeti vya hosptali ni sahihi.


Naona dili limebuma now Hanna kashikashi wilaya waliwataarifu uongoz mchezo wao.

Tetesi ni kuwa kuna viongoz walikula pesa za mabati ya hosptali mkurugenz akawaamuru walejeshe ndio wakatafuta njia hiyo ya kurejesha.
 
Kama ni kupigwa basi haizidi 5000 (kama ni kweli)

Huku kwetu ni 10000 ila unailipia bank
Unalipa za nini kwani vyeti vya kuzaliwa vinatolewa shuleni? Wakidai vyeti nenda NIDA katengenezewe cheti njoo nacho shuleni biashara imeisha.
 
Back
Top Bottom