Wizara ya Elimu iwasaidie wazazi katika hili waache kuibiwa

MR.NOMA

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
338
502
Wakuu habari!

Tukiwa tunaelekea mwezi Januari ambapo wazazi wengi wenye watoto wanaosoma sekondari watatakiwa kuhakikisha wanawanunulia watoto mahitahi yote muhimu ya shule kabla ya shule kufungua ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya masomo.

Sasa Kuna mahitaji mengine wanayoagizwa watoto wa kidato Cha kwanza unajiuliza kwanini Kila mwaka huagizwa au Kuna wajanja wanajinufaisha na bidhaa hizo.

Ninayoandika nimeyaona kwenye joining instructions za shule kadhaa za binasfi na umma pia. Mfano Mwanafunzi anatakiwa aje na:- Kwanja1, Jembe 1, Fagio laini 1, Fagio gumu 1, Sasa piga mahesabu kama wanafunzi wa kidato Cha kwanza wapo 100 hivyo shule itapata makwanja 100, mafagio 100, jembe nk. Kumbuka wale waliopo kidato Cha pili na wao walikuja na makwanja mwaka 2021 January,hivyo hivyo wale wa kidato cha tatu na nne nk.

Hivyo kama shule Ina wanafunzi mia 700 hivyo shule pia Ina mafagio 700, Makwanja 700, majembe 700 na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne au pia waliohama shuke majembe na makwanja Yao yanabakia shule. Haya ukija pia kwenye swala la rimu za karatasi.....kika mtoto aje na rimu 3 anapowasili shule....

Rimu hizo zitakabidhiwa Kwa mwalimu wa taaluma / MaKamu Mkuu wa shule. Haya kama kidato Cha kwanza wapo 100 x3 =rimu 300,hapo ni muhula wa kwanza tu huo muhula wa pili rimu 2 Kila mwanafunzi,hizi rimu zote ni kweli wanatumia wanafunzi husika au Kuna wajanja wanajinufaisha kwenye hili na kuwaibia wazazi?
 
Rimu zina kazi nyingi sana shuleni hatumii tu mwanafunzi kuna kazi nyingi sana zinafanywa kwakutumia hizo Rim

Kuhusu vifaa vya usafi kama mifagio na makwanja wanafunzi ni vinara wa kuiba au kuharibu hivyo vifaa hivyo huwa kuna upotevu mkubwa sana wa vifaa mashuleni
 
Vinavyopotea na kuharibika labda ni asilimia 10 tu, lakini kama umewahi kuwa mtunza store shule ya secondary basi utakuwa unajua vinaenda wapi vile vitu.
Vingi vinauzwa sana, majembe, ndoo, makwanja, ila vinaondolewa muda ambao hamuwezi kujua. Then siku wazazi wakihoji wanaletewa makwanja ya miaka mingi ambayo yalishachakaa au kuharibika.
 
mkuu kweli mtoto atumie fagio ,kwanja na jembe miaka minne na vibaki vizuri kweli.
 
Hivo vitu vinapigwa..
Nakumbuka m wakat nasoma oleva miaka ile nilipeleka vyote ivo lkn tangu nimeanza form 1-4 sikuwahi kutumia jembe jipya wala kwanja jipya vifaa vyote tulivyokuwa tunatumia vilikuwa used tunaambiwa vyetu vipo store tu
 
Back
Top Bottom