Wizara ya Elimu ishinikize vyuo vya Serikali vilipe madeni ya walimu wa part time katika kipindi hiki kigumu cha janga la COVID-19

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,144
15,144
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza tunaomba Wizara isaidie Vyuo Vikuu vya Serikali ambavyo vina tabia ya kulimbikiza madeni ya walimu wa part time vilipe mara moja hasa katika kipindi hiki cha janga la Corona ambapo kujikimu imekuw shida kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi kuathirika.

Nitatoa mfano wa chuo cha DIT ambapo toka mwaka huu uanze walimu wa part time bado wanadai malipo ya January na February na tunaelekea nusu ya mwaka sasa. Sio sawa kwa vyuo vya Serikali kutolipa walimu madeni ya nyuma kisa vyuo vimefungwa wakati inafahamika wazi hali ni mbaya mtaani pesa inahitajika kuendesha maisha katika kipindi hiki cha janga la corona.

Tunaomba Waziri wetu mpendwa na msikivu avishinikize vyuo hivi hasa DIT ambao mara kadhaa tabia hii hujirudia ama kwa uzembe wa mtu mmoja au kwa bahati mbaya.
 
Back
Top Bottom