Wizara ya Elimu ionyeshe uongozi katika kuchunguza masuala tata mashuleni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Elimu ionyeshe uongozi katika kuchunguza masuala tata mashuleni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 11, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni muda mrefu sasa matukio ya ajabu yamekuwa yakitokea katika mashule yetu.Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna hatua madhubuti zinazo chukuliwa kutafuta chanzo cha matatizo hayo na hatimaye kuyatafutia ufumbuzi.Jana tarehe 10 September 2008, tukio lingine la watoto waliokuwa wanafanya mtihani wa darasa la saba limetokea huko Tabora.Katika hali isiyoeleweka watoto hao walianguka na kupoteza fahamu.Hii sio mara ya kwanza.Kuna mwelekeo kwamba watu wengine wanahusisha matukio haya na matendo ya ushirikina ,lakini mimi sina uhakika ingawa inawezekana.Ushauri wangu ni kwamba wataalamu wa mwili wa mwanadamu wahusishwe kikamilifu katika kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo mbalimbali yanayotokea mashuleni.'Hormones' zote zinazohusika na 'human behaviour' ziangaliwe kwa undani.Kuna taarifa za kuaminika kwamba ipo mikakati ya makusudi ya kuharibu tabia za mwanadamu wa asili kupitia kwenye chanjo,madawa mbalimbali,vyakula,nguo nk..
   
Loading...