Sasa mkuu, unataka Wizara na taasisi zake, watoe video na audio kusomesha wanafunzi wa Feza kwa mfano?Wizara haimaanishi watu waliopo kwenye makao makuu ya wizara ya elimu pekee, wizara ya elimu ni kubwa kuliko hapo. Wizara inainclude taasisi nyingi ikiwemo vyuo vikuu vya serikali, VETA , taasisi ya elimu, NECTA n.k. Kabla ya kuhamishiwa TAMISEMI hata shule zote za serikali pia zilikuwa sehemu ya wizara ya elimu.
Kwa sasa hivi wizara bado inasimamia shule kwenye mambo mengi ikishirikiana na TAMISEMI ikiwemo mitaala na viwango na nadhani hapo ndipo mtoa mada anataka wizara kuplay part. Wanaweza kufanya kazi na walimu kuandaa media resources za kufundishia wanafunzi na kuanza na mahali kutumika mahali ambapo kuna miundimhinu ya msingi kama umeme na internet na kuendelea kuongeza network hadi kufikia shule zote.
Si lazima ifanyike yote kwa pamoja lakini inaweza kuchukua hata miaka kumi, ila la muhimu ni kuanza. Wakati itapofikia vijiji ambavyo kwa sasa hakuna internet/umeme tutakuwa tumeshaboredha media resources zenyewe, kutakuwa na walimu wenye uzoefu wanaoweza kufundisha na ku-share uzoefu na wezao na pia kutakuwa na wanafunzi wengu ambao walipata elimu bora kutokana na improvements za jinsi ya kufundisha.
Nafikiri utakuwa hujanielewa, Jukumu la kusomesha mwanafunzi sio la Wizara, ni la MWALIMU.