Wizara ya Elimu chunguze hizi shule za kata zilizo na bweni (Hosteli) ni mazalia hatari ya kuharibika wanafunzi

road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
2,064
3,011
Wahusika wa kufuatilia shule za bweni za kata ( hosteli) hili:

Kumeibuka utaratibu wa kuanzisha hosteli kwenye shule nyingi za kata hapa Tanzania ,lengo LA zoezi hiki ni zuru kwan hufanya wanafanzi wakae karibu na shule ile kuongeza ufaulu .

Lakini kuna haja wahusika kuweka utaratimu ili zoezi hilo liende kwa ufanisi mzuri !!

Zifuatazo ni hitilafu hatari sana ambazo nimezichunguza na kuona zaweza leta adhari kuwa hasa kwa wanafunzi wanaoishi ktk hosteli hizo

1) hayo mabweni yana mbanano usio wa kawaida!!!! Ili wahusika wapate kipato wanafunzi hulazimwishwa kulala wawili wawili kitanda kimoja ama watatu kutegemeana na body size ,hilo ni jambo LA hatari mno kiafya na ni rahisi kuibuka kwa usagaji na ulawiti miongoni mwa wanafunzi.

2) Wahusika yaani walimu huchukua wanafunzi wsliokwisha maliza kidato cha NNE waliofeli ili waje wasome wapate ( tuition) huku wakisubiri kurudia mitihami yao ya form four ,hili pia ni jambo LA hatari sana kwani majibaba hayo mengi hujikita katika mapenzi na wasichana wadogo walio katika mabweni! Ikumbukwe ili kuokoa harama wahusika hawaajiri matron na patron huchagua wanafunzi wenyewe wajisimamue hili ni balaa zaidi

3) Kutokuwepo vifaa vya kujikinga na hatari ya moto ni balaa jingine

4) Miundombinu isiyofaa ya mabweni ,haya mabweni yalikua ni madarasa hivyo hata milango na madirisha so ya kua bweni .Mfano mlango wa bweni wapasaw kufunguka kwa nje lakini milango ya madarasa hufunguka kwa ndani hapa ni hatari !! Madirisha ni nondo na wavu hivyo ni hatari kwa hadharura

5) kukosekana kwa uzio fensi hasa kwa mabweni ya wasichana tena wasio na matroni ni hatari zaidi.

Tafadhali wahusika fuatikieni hilo kupunguza hatari
 
Mimi naona ungeishauri Serikali yako sikivu kujenga mabweni ya kisasa katika shule zote za Sekondari za Kata nchini! Badala ya hizo fedha kuzichezea kwenye mambo yasiyo na tija kama kununua midege, kununua wapinzani, kununua Ma V8 ya kutembelea, nk.

Ila siyo kuwakatisha tamaa Wakuu wa shule na Wazazi walio amua kwa juhudi zao kujenga hayo mabweni ili kuwanusuru watoto wa kike dhidi ya mazingira magumu ya kupata elimu ya Sekondari.

Kimsingi shule za kata zina changamoto lukuki! Na hakuna Kiongozi anayejali. Kuanzia uhaba wa mabweni, madarasa, madawati, uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi, uhaba wa vitabu vya kiada na ziada, kubeba watoto wote kutoka shule za msingi na kuwaingiza sekondari hata kama hawana uwezo, nk.
 
Toa hiyo avatari ya baba wa taifa, hakuwa na mawazo mfu kama wewe
 
Back
Top Bottom