Wizara ya D. Kawambwa yateua "kihiyo" ukuu wa chuo

MWANIKO

Member
Oct 3, 2011
23
2
Mwezi Septemba 2011 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilifanya Uteuzi wa Wakuu wapya wa Vyuo nchi nzima-Tanzania Bara na kuwabadilisha vituo wengine ambapo miongoni mwa Wateule wapya ni Bw. MATHIAS MVULA ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu Mpya wa Chuo cha Diploma za Ualimu TUKUYU, MBEYA lakini pamoja na Uteuzi huo, kumekuwa na maneno ya chini kwa chini kuhusu Sifa na Uadilifu wa Bw.Mathias Mvula kama ifuatavyo:-
  1. Elimu ya Bw.Mvula ni Diploma ya Ualimu lakini pia kuna maelezo kwamba alijiendeleza kwa kusoma Open University of Tanzania(OUT) Shahada ya Ualimu ambapo kuhitimu kwake kuna Giza kutokana na maneno kuwa wakati huo (2008) Open University kulikuwa na Udanganyifu wa Mitihani, malalamiko ya Usahihishaji na mengine mengi.Hivyo hili linatia kiwingu juu ya uwezo wake Kitaaluma Bw.Mvula.
  2. Serikali haifanyi Biashara lakini kazi yake kubwa ni kutoa Huduma kwa Umma/Wananchi wake.Katika kipindi cha 2009-2011 Bw.Mvula alikuwa Chuo cha Ualimu Dakawa ,Morogoro ambapo akiwa hapo kulikuwa na malalamiko ya kuingiza chuoni Wanafunzi (Admissions) kwa Upendeleo nje ya Utaratibu wa Wazi wa Wizara ya Elimu na Wanafunzi wengine wakisikika wakisema waliombwa HELA ili kuingizwa Chuono.Hili suala linatia wasiwasi juu ya Uadilifu wa Bw.Mvula kwa Umma ikiwa atakuwa Muaminifu na mwadilifu katika Chuo cha Ualimu TUKUYU,MBEYA akiwa PRINCIPAL MPYA.
  3. Pia kwa mujibu wa Waraka wa MUUNDO wa Utumishi wa Wakufunzi katika Miundo ya Utumishi ya kazi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, toleo jipya la tarehe 10/8/2011 unaelekeza kuwa ili Mtu awe PRINCIPAL / Mkuu wa Chuo cha Diploma za Ualimu ni lazima awe Mkufunzi wa Chuo Daraja la I mwenye Shahada ya Uzamili (Masters) na Utendaji mzuri wa kazi kulingana na OPRAS lakini Bw. Mathias Mvula HANA SIFA HIZO zilizotajwa katika waraka ili kupewa Madaraka hayo.
HIVYO WADAU WA NCHI HII JADILINI HILO MAANA KUNA WATU NCHI HII WANAKULA KEKI YA TAIFA KWA MADARAKA MAKUBWA WAKATI SHULE ZAO ZINATIA MASHAKA MAKUBWA HUKU WALIOSOTA DARASANI WAKIWA WABEBA MAFAILI TU NCHINI MWAO.
 
hii ndio CCM zaidi uijuavyo!!! As long as jamaa anakula na wakubwa na ni kada 'mtiifu' wa CCM usishangae akawa hata Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu.
 
Huu sasa wivu

mijitu mingine ilifaa kuzikwa ikiwa hai!!! wivu ni nini hapo??? Kila post lazima iwe na minimum qualification na mtoa mada ame-refer waraka wa OR UTUMISHI lakini wewe unayefikiri kwa masabuli bado unapinga!!! Pumba fu kabisa!!!
 
Si unakumbuka hata Waziri mwenyedhamana uteuzi wake na utendaji kazi wake ulivyo na mashaka.
 
Hizo nyaraka huwa zinaandikwa lakini hakuna ufuatiliaji. We mgeni na hii nchi nini? Kwani wangapi wamedanganya elimu zao lakini bado wanaongoza chi hii tena ktk ngazi ya uwaziri. Hiyo ndo bongoland, we endelea na maisha mkuu, mitanzania na lirais letu ndo tulivyo
 
Huyo unamwonea tu na utaambulia dhambi bure,uanze na nyangumi wanaoimaliza nchi hii na ambao wameleta mfumo wakifisadi basi hata huyo atarekebishwa,kwa taarifa yako usizime moshi zima moto
 
Nionyesheni mahali gani na wizara gani katika nchi hii ambapo uteuzi hufanywa kwa kufuata sifa.
 
tuhuma zako dhidi ya mvulla ni za kufikirika sana, hatuwezi kuzitumia kumuhukumu kihiyo alifoji kuanzia chuo DIT, na vyeti ss sijui unamlinganishaje na huyu mvulla
 
ulikuwa unakaimu hapo? hebu tuwekee cv yake. Kama huna jinyamazie. udanaganyifu vyuo vikuu upo kila chuo.
 
Habari kwamba kuna Mkuu mpya Tukuyu ni njema sana kwangu!!!! Huyo jamaa aliyekuwepo alikuwa balaaa!!!
 
mijitu mingine ilifaa kuzikwa ikiwa hai!!! wivu ni nini hapo??? Kila post lazima iwe na minimum qualification na mtoa mada ame-refer waraka wa OR UTUMISHI lakini wewe unayefikiri kwa masabuli bado unapinga!!! Pumba fu kabisa!!!

unahangaika na form6 leaver, hata OR hajui ni nini. Achana nalo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom