Wizara ya Biashara iwe inatoa Bei Elekezi kwa bidhaa zote tunazoagiza nje wakati huu wa vita ya Russia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,854
141,792
Wafanyabiashara ni watu wajanja wajanja wanaweza kutumia tamko la Rais wa JMT kama fursa ya wao kupandisha bei za bidhaa kienyeti na bila uhalali wowote.

Nashauri Waziri wa Viwanda na Biashara aanze utaratibu wa kutoa bei elekezi kwa bidhaa zote.

Akipata ugumu wowote aende akajifunze kwa waziri wa biashara Zanzibar anaujua vizuri sana utaratibu wa bei elekezi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwahio tunapangiana Bei ?

Watu mnachangua upande kulingana na siku au dakika....., Issue na Story za Soko Huria zimeishia wapi ?
 
0116E2BA-972F-4AA1-B9D5-2D7A7E218105.jpeg
 
Pamoja na soko huria, serikali makini ni lazima ije na mkakati wa kudiscourage wafanyabiashara wenye tamaa kujipangia bei holela kwa visingizio kama hivi.
 
Kiukweli, ukienda kwny minada ya ng'ombe; Ng'ombe hawana bei kivile..lakini ukija buchani nyama haishikiki..samaki nazo bei juu mno, na haya yote ni mazao yetu ya ndani, wala hayapajui rashia
 
Wa buchani wamebanwa na ushuru na tozo za kila aina
Kiukweli, ukienda kwny minada ya ng'ombe; Ng'ombe hawana bei kivile..lakini ukija buchani nyama haishikiki..samaki nazo bei juu mno, na haya yote ni mazao yetu ya ndani, wala hayapajui rashia
 
Back
Top Bottom