Wizara ya ardhi tatueni hii migogoro kabla hajafa mtu kwa mapanga au kulogwa

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau..!

Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la 9 September kwamba muda si mrefu lile eneo lote la Kurasini-Temeke lilitwaliwa miaka kibao ya nyuma enzi za JK sasa litaanza kufanyiwa kazi kwa kugeuzwa kituo cha biashara.

Pia maeneo ya karibu yote na hapo kama Machungwa na Mivinjeni kumekuwa na migogoro kati ya wawekezaji wao kwa wao wakigombea maeneo mfano pale Mivinjeni kitu ambacho kimepekekea ugomvi mkubwa sana wa watu kutishiana mapanga ,na baadaye wazee wakaamua kufanya kikao cha kusoma albadili ili kuwaloga wote wanao muhujumu muwekezaji wao wanaomtaka wampatie eneo la kuwekeza baada ya kukidhi vigezo vyote vya utwaaji wa eneo.

Inasemekana kwamba mwekezaji mmoja alifuata taratibu zote za kutwaa eneo,wananchi wakajaza fomu zote wanachongoja ni malipo tu ila sasa kuna watu ndani ya serikali wakishirikiana na mwekezaji mwingine mwenye interest ndio wanaleta figisu figisu baada ya njia za kisheria kugonga mwamba sasa wazee wameamua kutumia majini ,maluani na mashetani kwa yeyote anayewahujumu.
 
Eneo gani hilo ?
Tatizo kubwa maeneo ya huko ni ulafi pia wa viongozi hasa wa mitaa..
Rushwa nje nje
Mivinjeni kuna mgogoro
Machungwa-Ruby kuna mgogoro yaani watu walafi sana wanataka wamweke mtu kati mwekezaji wao ndio wawe madalali wawe wananunua nyumba za wananchi kwa kubagain sio kwa kufuata taratibu za utwaaji wa maeneo.
 
Back
Top Bottom