Juzi tumesikia waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi amewaagiza NHC kutofanya jambo lolote isipokuwa analoagiza yeye kwa maana ya kupata idhini yake.
binafsi nimeshangazwa na agizo hilo kwa maana nikiangalia wizara na NHC kwangu mimi naona angalau NHC inatambua wajibu wake na imefanya kazi kubwa kutimiza wajibu wake katika miaka ya hivi karibuni. matatizo yanaweza kutokea kutokana na mabadiliko ya kisiasa ambayo yanaathiri uchumi pia.
lakini kwangu mimi wizara isiyojua wajibu wake na isiyotekeleza ni wizara hii ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi.
wataalamu wanasema maendeleo ya kwanza katika mji ni mpango wa makazi kwa maana makazi yanapangwa ili kuwapatia wananchi huduma kwa urahisi, kulinda mazingira na mambo mengine.
mijin yetu yote nchini inazidi kuvuriga watu wanajenga ovyo, wizara hii badala ya kupanga miji yetu ili kumletea mwananchi maendeleo inaonekana kutokutambua wajibu wake.
wao wanadhani jukumu lao ni kuhalalisha viwanja na matokeo yake ni makazi ya watu kuchanganyika na shughuli za kiuchumi zisizostahili kukaa katika makazi ya watu mfano viwanda, hawapangi miji kubainisha maeneo yanayostahili kulindwa kwa ajili ya mazingira bali kutoa matamko jumla ya mabonde, makazi ya watu yanakosa huduma muhimu kama usafiri.
watu wengi wanadhani kushamiri kwa boda boda ni maendeleo bila kuangalia kuwa hili ni tatizo la mipango miji inayomlazimisha mtu kutumia gharama kubwa katika usafiri.
kutokupanga miji kumesababisha miji kusambaa kwa kasi sana na kufanya kazi ya kuwapa huduma za kijamii kama hospitali, masoko, shule kuwa ngumu. kutokupanga miji kumesababisha jamii kukosa maeneo ya huduma hizi. wakibahatika kupata eneo la kujenga shule hakuna eneo hata la viwanja vya michezo.
tunalaumu kutokufanya vizuri kwenye michezo kumbe tatizo la msingi limekaa kwenye wizara hii kutotimiza wajibu wake.
tatizo hili limetoka mbali huko nyuma lakini hiyo ni sababu ya kuliacha liendelee na kuwa kubwa zaidi au ni wakati wa kusema yaliyopita yamepita kwa sasa tunaweka mwelekeo mpya.
sasa watu hawa walioshindwa majukumu yao wanadhani majukumu yao yote wanayatimiza vizuri na yamekwisha na wanaweza kupata kupata mda wa kushughulikia mambo ya kiutendaji ya NHC.
je tutafika? huwa anauliza jamaa mmoja kwenye kipindi cha tv
wizara hii inadhani kupima ni wewe kuja kwao na kuomba wakaleta wataalamu kuja kupima eneo ukalipa gharama wakakupa hati. eti hiyo ndio maana ya kuondoa squarter kwao bila tofauti ya msingi kwa maana ya kuangalia jamii yote kwa pamoja bali tofauti ni hati ?????
hoja yangu kati ya Wizara hii na NHC ni nani unadhani amelala usingizi fofo wa kustahili kuamshwa?