National Council of Professional surveyors NCPS ndiyo yenye mamlaka ya usajili wa wapima ardhi (Land Surveyors) na wathamini ardhi (Valuation/economy surveyors). Bodi hii imekuwa dormant kwa zaidi ya mwaka. Kisa waziri aliyekuwepo Prof Ana Tibaijuka alishindwa kuteua mwenyekiti. Na baadae Mh. LUKUVI akarithi nafasi hiyo naye ameshondwa kuteua m/kiti. Wazo alilolitoa la kukataa kumthibitisha m/kiti kwa kigezo kuwa ni mtumishi wa umma na hivyo kutakuwa na mgongano wa kimaslahi ni zuri, hata hivyo haliendani na sheria iliyopo sasa. Watalaam hawa wa ardhi hasa wale wenye kiu ya kusajiliwa wamekuwa gizani kwa kipindi kirefu kama kondoo wasio na mchungaji. Je katika hili wizara ya aedhi nani jipu?