Luhaga Mpina kudaiwa kudhulumu ardhi ya Kijiji ekari 1000 Morogoro, Wizara ya Ardhi iingilie kati

Duh...!. Sasa ndio mnaanza kufurumua ya Mpina kwasababu tuu amemsema JM?. Siku zote mlikuwa wapi?!.
P
Wakifumuana ndio nafuu Kwa Watanzania, tujue madhambi ya watawala...Bila kujali ni lini wamefurumua...KATIBA MPYA ni muhimu

Yaani wanakalia ardhi kubwa, akina Mkapa, Mwinyi, Sumaye...mpina, na wengine...kisa wanayo vijisenti walivyokula rushwaa!

Badala ya kulima Alizeti na Karanga, mafuta yapatikane Kwa wingi... wapewe wananchi, walime Alizeti

Badala yake, Mafisadi wanahodhi ardhi..kupiga picha na kunya humor tu
 
Hii ni sheria, Serikali ya Kijiji haiwezi kugawa ardhi yenye ukubwa wa ekari zaidi ya 50! Wizara ya ardhi, Mpina anasema kapewa ekari 1000 na Kijiji, japo Kijiji wanakataa kumpa ardhi ya ukubwa huo!

Sheria zisimamiwe, huyu amevunja sheria, anyanganywe hiyo ardhi iliyozidi ekari 50, arejeshe ekari 950!

Wizara ya ardhi iingilie kati kuokoa ardhi ya Kijiji!
Weka nukuu ya kifungu cha sheria hiyo mkuu.
 
Hii ni sheria, Serikali ya Kijiji haiwezi kugawa ardhi yenye ukubwa wa ekari zaidi ya 50! Wizara ya ardhi, Mpina anasema kapewa ekari 1000 na Kijiji, japo Kijiji wanakataa kumpa ardhi ya ukubwa huo!

Sheria zisimamiwe, huyu amevunja sheria, anyanganywe hiyo ardhi iliyozidi ekari 50, arejeshe ekari 950!

Wizara ya ardhi iingilie kati kuokoa ardhi ya Kijiji!
"Migambo wanaruka na kukanyagana" repeat Chorus
 
Duh...!. Sasa ndio mnaanza kufurumua ya Mpina kwasababu tuu amemsema JM?. Siku zote mlikuwa wapi?!.
P
Tulishaanza siku nyingi, lile dubwana lilimlinda, sasa veil inafunuliwa kirahisi, japokuwa iko transparent
 
Morogoro. Wakati wananchi wa kijiji cha Dala kata ya Mvuha mkoani Morogoro wakimwomba Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia kurejeshwa kwa ekari 700 zinazomilikiwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, mbunge huyo amekiri kumiliki ardhi hiyo kihalali.

Mgogoro huo ulioulianza tangu mwaka 2009 baada ya Mpina kumilikishwa ekari 300 na mkutano wa kijiji.

Alipoulizwa leo kwa simu, Mpina alikiri kumilikishwa ardhi hiyo na Serikali ya kijiji na amedai kuwa baadaye baadhi ya wajumbe wa kijiji wakajigeuza kuwa mashamba ni ya kwao.

“Hizo ekari nazimiliki kihalali na fedha kwenye akaunti niliziweka kihalali, ndio maana hata alipokwenda Mkuu wa Mkoa na Wilaya kilichokubalika ni kupima eneo.

“Sasa kiustaratibu katika upimaji kisheria huwezi kuingia kwenye kulipima eneo bila kukamilisha kesi iliyokuwa inaendelea,” alisema.

Wakizungumza katika mkutano wa kijiji uliofanyika jana Aprili 9, wanakijiji hao wamedai kuwa mbunge huyo amejimilikisha ardhi yao kinyume na utaratibu.

Mkazi wa kijiji hicho, Kadiri Omary akizungumza katika mkutano huo, amesema mwaka 2009 akiwa mjumbe wa Serikali ya Kijiji, Mpina aliomba kupewa hekari 300 na kupatiwa na kijiji hicho.

Amesema ilipofika 2016 Mpina aliomba kumiliki ardhi hekari 700 ili awe na ekari 1,000 ambapo mkutano mkuu wa kijiji ulikataa maombi yake na kumtaka asitumie ardhi yao.

Omary amesema lakini kutokana na mamlaka aliyokuwa nayo kwa wakati huo aliweka walinzi na kuendelea kufungua mashamba katika ardhi ya kijiji bila ridhaa ya wananckijiji.

Naye Abubakar Kiwembela walimlalamikoa kiongozi huyo bila mafanikio katika Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kwa CCM.

Amesema walilazimika kufungua shauri namba 54 la mwaka 2018 katika Baraza la Ardhi la Wilaya ambalo walishinda na kutakiwa kupatiwa eneo hilo.

Kama hiyo haitoshi, amesema walifungua maombi ya kukazia hukumu namba 410 ya mwaka 2022.

Maelezo hayo yameungwa mkono na mwanakijiji Idd Kibwana aliyesema kuwa, mwaka 2018 mgogoro ukiwa na miaka saba wananchi walifikisha malalamiko yao kwa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally ambaye aliwapa matumaini kwa kuahidi kushughulikia suala lao lakini halikuzaa matunda.

“Agosti 2018 Mwananchi lilichapisha kuwa Dk Bashiru kupambana na waziri anayemiliki ekari 1,000 (wakati huo Mpina alikuwa Waziri wa Mifugo na uvuvi), lakini pamoja na kauli hiyo hatukuona lolote,” amesema Kibwana.

Ameendelea kusema kuwa malalamiko hayo waliyafikisha kwa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Willium Lukuvi kupitia kikao cha Baraza la Madiwani cha Agosti 30, 2018 ambapo bado Mpina aliendelea kutumia ardhi bila ridhaa ya wananchi wala maridhiano.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mohamed Kilimasinde amekiri Serikali ya kijiji kumpa Mpina ekari 300 za awalia lizoomba mwaka 2009 lakini baada ya hapo alinyimwa ekari 700.

Amesema mwaka 2009 alifika kijiji hapo aliomba ekari 300 na kupata baada ya kujadiliwa na Serikali ya kijiji na kwenye mkutano kuu.

Amesema mwaka 2017 uongozi wa Mkoa, wilaya, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya walifika kijijini ili kufahamu hitimisho ambapo ilionekana serikali ya kijiji ilikuwa na makosa kuidhinisha ekari hizo za awali.

Kilimasinde amesema wakati huo Mpina alikuwa ameweka kwenye akaunti ya kijiji Sh35 milioni alizosema zitatumika kwa shughuli ya maendeleo.

Diwani wa kata ya Mvuha Mfaume Chanzi amesema mambo yote yaliyozungumzwa atahakikisha anayafikisha ngazi zinazohusika ili kushughulikiwa kwa haraka.

Source, gazeti la @Mwanachi
 
mwisho wa yote unahitaji kisehemu kidogo tu kuzikwa. tamaa za nini? na ukute hiyo ardhi anataka akae nayo tu kama sehemu ya mali zake, hakuna la maana analofanyia.
 
Makaburi haya yanafufuliwa maana Mpina kaishambulia CCM.
You scratch my back, I scratch yours.
 
Luhaga Mpina, Vita aliyoianzisha, ahakikishe ana nyundo na silaha za kutosha,
Akiwa kiongozi alijua sheria za ardhi, kijiji hakiruhusiwi kutoa zaidi ya ekari 50.

Yeye alipataje hizo 300 kupitia kijiji!?

Ngoja maCCM wavuane nguo! Picha linaanza!
Kila mzalendo tuonyeshwe uchafu wake!
 
Siyo kijiji hakiruhusiwi kutoa zaidi ya 250? Lakini wameshamdaka.
 
Naona wana CCM wenzangu tumeanza kushambuliana kisa tu tunaowapenda wameshambuliwa.

Nahimiza wanachama wa CCM kusimama imara kutetea haki ktk taifa letu la Tanzania.

Tukemee rushwa na dhuluma kwa yeyote yule ndani ya chama na nje chama.

Taifa mbele, haki mbele, vyama baadaye
Umemena vema mkuu
 
Back
Top Bottom