Wizara ya Ajira wateuliwe wasomi waliofanikiwa kutengeneza ajira kupitia elimu zao

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,318
8,228
Huu ni ushauri:

Napendekeza

Wizara ya ajira wateuliwe wasomi waliofanikiwa kutengeneza ajira kupitia elimu zao.

Serikali isitishe kuteua mawaziri watafuta ajira katika hii wizara nyeti.

Wanakosa ubunifu kwasababu wanakua hawana uzoefu wala ujuzi unaoweza kusaidia kuwapa uelekeo watanzania.

Kutoa ajira sio kutoa mikopo tu, kuna kufundisha pia jinsi ya kuutumia mkopo. Pia kuna kuwaelekeza vijana maeneo yenye fursa ili vijana waweze kujiajiri huko.

Serikali inapoteza nguvu kazi, kwa kukosa walimu wa kufundisha hayo. Vijana wanamorali ya kufanya kazi Ila wanakosa motisha.

Ni wakati wizara hii itengewe watu maalum sana, isiteue tu.

Kama tunaona msomi katengeneza ajira tumchukue tumpe hiyo nafasi ili asaidie taifa.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom