Wizara ya Afya yawatahadharisha Watanzania kuhusu ugonjwa wa Homa ya Uti wa Mgongo

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ulijitokeza katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC).

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt.Aifelo Sichwale amesema ugonjwa huo wa mlipuko husababishwa na bakteria wanaojulikana kama 'Neisseria Meningitides'.

Taarifa ya Dkt.Sichwale kwa vyombo vya habari ianeleza kuwa ni vyema tahadhari kuendelea kuchukua kwani magonjwa hayana mipaka, hususani mikoa inayopakana na DRC.

Aidha Vimelea vya ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au kukaa na mtu mwenye maambukizi, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Septemba 8, 2021 na Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, mlipuko huo unaoambukiza ni tishio kwa sasa Barani Afrika.

20210916_233020.jpg
20210916_233023.jpg
 
Serikali imewataka Watanzania kuchukua tahadhari kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo uliotokea katika jimbo la Tshopo nchini DRC Congo.

Vimelea vya ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au kukaa na mtu mwenye maambukizi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Septemba 8, 2021 na Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, mlipuko huo unaoambukiza ni tishio kwa sasa Barani Afrika

Taarifa iliyotolewa Septemba 16, 2021 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichwale, imesema ni vyema kuendelea kuchukua tahadhari kwani magonjwa hayana mipaka, hususani mikoa inayopakana na DRC.

Dk Sichwale amesema ugonjwa huo wa mlipuko husababishwa na bakteria wanaojulikana kama ‘Neisseria meningitides’.
“Ugonjwa huu huchukua siku mbili hadi 10 tangu kuambukizwa hadi kuanza kuonyesha dalili,” amesema Dk Sichwale.

Dalili
Dk Sichwale amesema dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na homa kali, kichwa kuuma, kutapika, kuogopa mwanga, kuchanganyikiwa na shingo kukakamaa.

Amesema ugonjwa huo unaweza sababisha madhara makubwa kwenye ubongo, kupotea kwa usikivu au ulemavu mwingine wa kudumu na hata kupoteza maisha.


Mwananchi
 
Aisee naona vifo vimekuwa vingi sana na Kuna wengi wanaambiwa tatizo ni uti wa mgongo, isije ikawa hii kitu ndiyo inafyeka watu Sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom