Wizara ya afya yawakomoa watoto wa wakulima tanzania!

FORESEER

Senior Member
Aug 1, 2013
111
15
Jamani leo nashuka jukwaani nikiiangazia macho Wizara ya Afya-Tanzania!
Kwa hali isiyo ya Kawaida kwa watoto wa WAKULIMA wameshindwa kuripoti vyuoni kwa kushindwa kulipa ada katika vyuo walivyo chaguliwa kujiunga katika mwaka huu wa masomo badala yake wanafunzi waliokwisha ripoti ni sawa na asilimia 35% katika vyuo walivyo pangiwa na asilimia 65% mpaka sasa hawajaripoti kutokakana na kupandishwa kwa ada katika vyuo mbalimbali vyilivyo chini ya WIZARA YA AFYA na hasa wengi wao wakiwa ni watoto wa WAKULIMA!

Kimsingi ada imepanda kutoka laki nane hadi milioni moja na thelathini na saba kiasi na gharama hizi zimepanda gafla bila hata kuwashirikisha wadau husika.
Hivyo wito wangu kwa Waziri wa Afya mh. Dr. Hussein Mwinyi tafadhari jaribu kuingilia kati suala hili ili hata watoto wa wakulima wanufaike na Elimu hii ndani ya nchi yao na si kufanya vyuo hivi kama MRADI WA KUJIPATIA PESA na Wizara ya Afya.
 
Back
Top Bottom