Wizara ya Afya yapiga marufuku watu kuzikwa usiku, yaagiza ndugu washirikishwe

Nadhani kigogo si mtu wa kupuuzwa, nadhani ni mtu muhimu Sana, analeta friction Kati ya wananchi na wafanya maamuzi wa serikali.
Kisayansi friction ni muhimu Sana ili kusogea kwenye uso wa aridhi. Au nyuso nyingine (surfaces)

Ili taifa lisogee linahitaji friction.

Asante kigogo I wish utengeneze taasis, hivi vyama pinzani Kwa sasa havina Meno kazi Yao unafanya wewe.

Note, uwe mzalendo

Mwisho: declaration of interest, naamini katika logic
 
Hili swala ni mpaka Rais aongee ndo Wizara ifanyie kazi? Tunampa Rais mzigo mkubwa kutokana na wateule wake kushindwa kujiongeza. Swala limelalamikiwa wiki kadhaa bila kufanyiwa kazi leo ghafla baada ya hotuba ya Mh Rais watu wanaamka. TZ tuna safari ndefu
 
Nitoke nje ya mada.

Hatuwezi kuongozwa na wanasiasa kwenye hiki kipindi kigumu kisha tutarajie kuushinda huu ugonjwa.

Ingekuwepo kamati ya wataalamu wa afya na majanga ingekuwa heri mihemko na hisia zingepungua.

Ni kosa mawaziri, wabunge na Rais wawe ndiyo wasemaje wakuu. Hawa kazi yao ilikuwa kupokea ripoti kutoka kwa kamati ya wataalamu.

Wao wanajua walau kila kitu kuhusu magonjwa...hawana mihemko...hawana chuki...wala hawana mirengo ya kisiasa wanasimamia miiko ya kazi.
Tatizo huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuambieni mpaka sasa mmeishazika wangapi usiku , au ndio wale famba 16 mnaotutangazia siku zote ?
 
Hili swala ni mpaka Rais aongee ndo Wizara ifanyie kazi? Tunampa Rais mzigo mkubwa kutokana na wateule wake kushindwa kujiongeza. Swala limelalamikiwa wiki kadhaa bila kufanyiwa kazi leo ghafla baada ya hotuba ya Mh Rais watu wanaamka. TZ tuna safari ndefu
umeamua kumpamba tu huyo mtu wenu huku ukijua wazi kwamba yeye ndio kikwazo , haya na wewe unataka kuteuliwa kwenye nini ?
 
Watuambie kwanza kabla ya tamko hili la kipuuzi ...watuambie kwanza waliozikwa usiku mpaka sasa ni wangapi na waliozikwa mchana wangapi
 
Lakin afadhali kwa sasa maana ilikua imezd kukithiri siku baada ya siku

Its not over until its over...
Lkn unadhani wataacha kuzika usiku?. Kwa kuangalia mentality ya rais kwa janga hili ni kuwa corona ni kaugonjwa kadogo kasiko sababisha mauti kwa wengi. Sasa vifo vikiongezeka kupitia observation ya wanao zikwa kwa siku, rais ataonekana "mwongo". In short, kuzika usiku ni mwendelezo wa kuficha taarifa. Hujashangaa waziri wa katiba kutumwa kuichunguza maabara ya taifa?
 
Kama hili agizo litatekelezeka basi watanzania mtajua hali halisi ya watu kufa kwa COVID-19. Muda utasema yote.
 
Watanzania hawana utamaduni wa kuzika wapenzi wao usiku wa manane ila kwa maagizo toka juu inaonekana Awamu hii iliamua kuchukua jukumu la kuzika wafu usiku kukwepa utamaduni uliokuwapo wa mtu yeyote asiyefika kwenye mazishi hutengwa na akifariki hususiwa kuzikwa. Kuzika usiku ni rahisi kupata watu chini ya 10 wa kumzika kila mfu kama Serkkali ilivyotaka. Kwa uamuzi huu mpya utashuhudia maelfu ya waombolezaji wakishiriki kila mazishi.
Waache waje kuomboleza, mbona makanisani, misikitini watu wanafurika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wale wajinga waliokuwa wanasema zile picha na video za watu kuzikwa usiku siyo za Tanzania. Wanajisikiaje saiv?
 
Nadhani kuna mambo mengine ya hovyo yanafanywa na Serikali, wengi tukiamini yamekubaliwa au ni maelekezo ya Rais, kumbe ni maamuzi wa baadhi ya watendaji wenye akili ndogo ndani ya Serikali...
Sasa wewe kama mambo ya hovyo na hayana mkono wa Raisi mbona serikali hiyohiyo ilikuwa inapinga kwamba watu hawazikwi usiku?
 
Back
Top Bottom