Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Wizara ya Afya imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii inayozunguka mitandaoni kuwa, mtaalamu wa Afya katika kituo ambacho bado hakijatambuliwa amemshona mgonjwa jeraha kisha akalifumua kwa madai kuwa mgonjwa huyo hakuweza kulipia gharama. Ikiwa hili limetokea nchini Tanzania, basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu. Hivyo, wizara inaomba wenye taarifa za wapi huku au kituo gani wawasilishe mara moja kwa namba ya huduma kea mteja 199 ya wizara ya afya au watume ujumbe mfupi kwenye namba ya waziri wa Afya ya 0734124191.