Wizara ya Afya yakanusha kuwepo kwa virusi vya ugonjwa wa Zika

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
717
1,000
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekanusha taarifa za kuwepo kwa vurusi vya ugonjwa wa zika nchini.

Katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo ametoa ufafanuzi huo na kukanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa huo, huku akirejea kauli yake kuhusu ugonjwa huo aliyoitoa mwezi Februari mwaka huu kuwa ugonjwa huo haujaingia nchini.

Kuhusu utafiti uliofanywa na Taasisi ya NIMR, amesema kuwa utafiti huo ulifanyika nchini kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya zika na chikungunya.

Amesema kwa utaratibu wa kitafiti hiyo ni hatua ya awali ya kuangalia ubora na uwezo wa kipimo hicho na kwamba matokeo yake bado yanahitaji kuchunguzwa kwa kina kupitia vipimo vilivyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani.

Taarifa hiyo imesema kuwa wizara kwa kushirikiana na taasisi na ndani na nje ya nchi inaendelea na utafiti na ufuatiliaji wa kitaalamu ili kuzuia ugonjwa huo kuingia nchini na tayari imeshaandaa mkakati wa zika ambao unaelekeza utekelezaji wa ufuatiliaji wa zika.

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini, (NIMR) iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari kupitia mkurugenzi wake Dkt. Mwele Malecela ilisema kuwa Tanzania ina wagonjwa wa zika ambapo asilimia 15.6 ya watu waliopimwa kati ya mwaka 2015 na 2016 walibainika kuwa na virusi vya ugonjwa huo.
 

balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
8,749
2,000
Mkurugenzi wa NIMRI dk Mwele Malicela anasema wamefanya uchunguzi na kugundua ugonjwa huo upo Tanzania,Ummy Mwalimu na Hamis Kigwangala wanasema haupo.Ni nani yuko sahihi?
 

Mwanitu

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
910
500
Mkurugenzi wa NIMRI dk Mwele Malicela anasema wamefanya uchunguzi na kugundua ugonjwa huo upo Tanzania,Ummy Mwalimu na Hamis Kigwangala wanasema haupo.Ni nani yuko sahihi?
Kama kweli umeingia hatua za dharura inabidi zichukuliwe ungali Kwenye eneo Dogo.Tukumbuke Ebola,kama Nchi za West Afrka zisingejitahidi kuuzibiti mapema hali ingekuwaje kwa sasa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom