#COVID19 Wizara ya Afya: Watanzania 207,391 wamepatiwa Chanjo ya UVIKO-19 hadi Agosti 14, 2021

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
32ad3e97-158c-447e-ba40-90ecb957001d.jpg
 
Hizi taarifa japo serikali wanazitoa niwapongeze lakini bado ziko nusu nusu, hatuambiwi wagonjwa wako wangapi, waliofariki wangapi, waliopona wangapi, serikali inachagua tu zile taarifa wanazopenda wao.
 
Bado mwamko ni mdogo sana yaani pamoja na kuonekana na kuaminishwa kuwa watanzania wengi wanahitaji chanjo bado hadi leo chanjo million 1 zinatuhenyesha namna hiii?

Hivi hizi chanjo hazina muda wa kuharibika? ni za muda gani hadi kuharibika?
Hao wanaohamashisha wanahamasisha nini ikiwa hadi leo hata nusu ya chanjo hatujaifikia?
 
Bado mwamko ni mdogo sana yani pamoja na kuonekana na kuaminishwa kuwa watanzania wengi wanahitaji chanjo bado hadi leo chanjo million 1 zinatuenyesha namna hiii?
Hivi hizi chanjo hazina muda wa kuharibika? ni za muda gani hadi kuharibika?
Hao wanao hamashisha wanahamasisha nini ikiwa hadi leo hata nusu ya chanjo hatjaifikia?
Watu wanakataa kwa kuamini vitu visivyokuwepo. Ujinga pia upo. Ni shida sana. Eti anaamini chanjo ni njama za mabeberu kutuangamiza.
 
Usifanye mchezo kuchanja watu laki mbili ndani ya siku 10 wewe jamaa kwa miundo mbinu tuliyonayo!!
 
Hatujafika robo ya chanjo zilizoletwa.

Akina Steve Nyerere waongeze uhamasishaji!
Kitendo cha Steve Nyerere kupewa ubalozi wa chanjo hii ndo kinachoepelekea watu kutotilia maanani chanjo! Alikosekana mtu mwenye haiba na ushawishi kuteuliwa balozi wa chanjo?! Ona sasa, watu wanaona chanjo kitu cha hovyo kwa kuwa tuu balozi wake ni mtu wa hovyohovyo
 
Leo naona hawajaweka mi-bold kwenye tangazo lao, ujumbe wa member mmoja wa JF uliwafikia!
 
Hizi taarifa japo serikali wanazitoa niwapongeze lakini bado ziko nusu nusu, hatuambiwi wagonjwa wako wangapi, waliofariki wangapi, waliopona wangapi, serikali inachagua tu zile taarifa wanazopenda wao.
Ni kweli kabisa kuna uhitaji wa kutoa taarifa za idadi ya wagonjwa wa COVID-19
 
Watu wanakataa kwa kuamini vitu visivyokuwepo. Ujinga pia upo. Ni shida sana. Eti anaamini chanjo ni njama za mabeberu kutuangamiza.
... mahali palipotamalaki ujinga ni shida Mkuu! Badala ya kupambana CCM wameamua kulea mama wa wale maadaui wakuu; UJINGA. Penye ujinga uliokithiri ni shida sana no wonder imani za kishirikina na kuamini uzushi kuliko ukweli vimetamalaki kona hii ya dunia.
 
Back
Top Bottom