Wizara ya Afya, tunasubiri bei elekezi ya dawa

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
880
327
Salaam wana jamvi!

Salamu hizi pia zimfikie mwanachama mwenzetu mh naibu waziri @HKigwangalla

Katika gazeti la mwananchi la tarehe 13 Novemba kulikuwa na habari ambayo sehemu yake ni hii hapa
“Ule wizi wa dawa tunataka ufikie ukomo, ndiyo maana tumeanza utaratibu wa kuweka alama ya TOG katika dawa zetu na tumefanikiwa kwa asilimia 50 hadi sasa, na asilimia iliyobaki tuna imani hadi mwakani itakamilika,” alisema Dk. Mmbando.
Alisema Serikali pia ina mpango wa kutoa bei elekezi ya matibabu katika hospitali za binafsi na za Serikali ili kila mwananchi aweze kumudu gharama hizo.

Sasa tunasubiri hizo bei elekezi maana huku mtaani kwetu dawa kama hizi hapa

1451897502951.jpg

Ni sh 5000....tu
Hali si nzuri
1451898372796.jpg

Ni dawa za kutuliza maumivu,paracetamol za siku 3

1451898484939.jpg

Nawasilisha!
 
Mkuu nashindwa hata nichangie vipi...jana Hospital ya sinza ilitaka kuniulia mama na mtoto...ngoja nikae vizuri nitakuja na uzi hapa wa tukio zima...
 
Mkuu nashindwa hata nichangie vipi...jana Hospital ya sinza ilitaka kuniulia mama na mtoto...ngoja nikae vizuri nitakuja na uzi hapa wa tukio zima...
Pole sana mkuu.
Hii biashara kwenye afya za watu itagharimu maisha ya wengi
 
Salaam wana jamvi!

Salamu hizi pia zimfikie mwanachama mwenzetu mh naibu waziri @HKigwangalla

Katika gazeti la mwananchi la tarehe 13 Novemba kulikuwa na habari ambayo sehemu yake ni hii hapa

Sasa tunasubiri hizo bei elekezi maana huku mtaani kwetu dawa kama hizi hapa

View attachment 314743

Ni sh 5000....tu
Hali si nzuri
View attachment 314745

Ni dawa za kutuliza maumivu,paracetamol za siku 3

View attachment 314746

Nawasilisha!
Tatizo kubwa la watanzania KILA MTU DAKTARI.Yaani yeye huyohuyo ndio DAKTARI(anajifanyia prescription na diagnosis huyohuyo),MGONWA HUYOHUYO na MFAMASIA huyohuyo anajiendea duka la dawa ambalo kwa hapa Tanzania wengi wao wanaouza si wataalamu wanamuuzia anaenda kumeza.Akipata madhara ANALAUMU SERIKALI.Kwanini msiende HOSPITALI MKASIKILIZWA NA KUFANYIWA VIPIMO ILI KAMA PHARMACY ZA SERIKALI HAKUNA DAWA MKANUNUE KWENYE MADUKA YA MSD KWA BEI NAFUU.........................
 
@Mkaruka
Hii taarifa inahusu bei ya dawa katika hospitali binafsi, vituo hivi vipo vingi na vipo karibu na makazi ya watu hivyo husaidia wananchi wa maeneo hayo.
Angalizo langu ni usimamizi kwasababu hawawezi kujiamulia tu wauze dawa kiasi wanachotaka.
Kuna dharula pia, wakati mwingine huduma ya umma ipo mbali na mgonjwa ni mahututi
 
KANUNI NA TARATIBU ZA UNUNUZI
1. Bei zilizopo katika kitabu hiki ni kwa ajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati za serikali pamoja na mashirika ya huduma yasiyo ya kiserikali (NGOs), hospitali za mashirika ya kidini (FBOs) zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

...
PARACETAMOL TABS 500 MG 1000 TABLETS TSH 7,000

source: MSD Catalouge 2013
 
Back
Top Bottom