WIZARA YA AFYA TUNAOMBA MTUSAIDIE KWA HILI TUMECHOKA

size 96

Member
Aug 31, 2019
95
150
wakuu poleni na majukumu nimeleta uzi huu nikiwa naimani wahusika wapo ambao wanatumia jf
Wilaya ya chunya ni moja ya wilaya kongwe Sana apa nchini lakini chakushangaza hospitali yetu haifanyiwi maboresho yanayo endana na hadhi ya wilaya yetu huduma za hospitali yetu ni mbovu mno wafanyakazi wa hospitali hii wanafanya kazi kwa mazoea Sana serekali yetu ya sasa inasema imeboreeha upatikanaji wa dawa lakini kwa hospitali yetu ni tofauti Sana kwani dawa baadhi tu ndo hupatikana gharama za matibabu zipo juu Sana
Majengo na miundo mbinu hafifu ya hospital
Huduma mbovu zinazo tolewa
Tunaomba watu wanao husika waje kutatua kero za wanannchi wa chunya
 

mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,470
2,000
ndugu yangu ikiwa huku dar wizara tunayo huku huku na rais tunae hapa hapa lakin huduma kwenye hospitali za serikali ni majanga sasa unazani mikoani kuna hali gani
 

charrote

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
914
1,000
Kama mazingira ya kaz ni mabovu unataka hao wafanyakaz wafanyej? Kama dawa hakuna watoe hela mfukoni wakununulieni dawa? Gharama za matibabu zimepangwa na Serikali hakuna hospital inayojipangia gharama.. Lia na awamu ya tano!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom