Wizara ya Afya; Nini maana ya matibabu bure kwa watoto na wazee?

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
10,257
12,929
Kwa wasio kuwa na bima:
Unaenda hospitali ya serikali na mtoto chini ya miaka 5 unaambiwa utoe hela ili upate matibabu,
Mzee ambaye ni zaidi ya miaka 60 anaenda hospitali anaambiwa bila hela hahudumiwi.

Je, nini maana ya matibabu bure kwa watoto chini ya miaka 5 na wazee zaidi ya miaka 60?
 
Nchi ya viwanja ,lakini bila masoko wala uhusiano mzuri wa kimataifa na biashara !!
Mkuu akiwaona mabalozi wamekuja anajifungia chooni
 
Kuna wazee walinieleza walipewa kadi za kuwasaidia wazee kupata matibabu bure kwenye hospitali ya wilaya. Chaa ajabu wakifika kule wanawekwa kwenye bench lao, daktari anawaona baada ya waliolipa wote kumalizika, hiyo inakuwa saa kat ya saa saba na saa nane mchana. Dawa wanazoandikiwa sasa, hujamaliza kujieleza tayari prescription ina paracetamol. Wanaona ni kheri tu walipe wahudumiwe kama wengine.
 
Hii mada angeleta mwingine najua wewe ungelikuwa wa kwanza kusema ni upinzani anapingana na serikali tukufu. No wonder imeletwa na wewe shabiki mkuu. Muda bado vumilia tuu na chanjo ya manjano nayo sahivi unapaswa ulipie 55000tzs utaki hama nchi. Hizi mada za kichochezi uache, hii ni serikali tukufu ya viwanda.
 
au mtu amemuhack Mudawote jamani
 
Ni hospitali gani yalipotokea hayo?

NI VILAZA TU WANAOPENDA KUGENERALIZE MAMBO
 
Kwa wasio kuwa na bima:
Unaenda hospitali ya serikali na mtoto chini ya miaka 5 unaambiwa utoe hela ili upate matibabu,
Mzee ambaye ni zaidi ya miaka 60 anaenda hospitali anaambiwa bila hela hahudumiwi.

Je, nini maana ya matibabu bure kwa watoto chini ya miaka 5 na wazee zaidi ya miaka 60?
UZI WA GAMBA UMEDODA
saa mzima wachangiaji 15?
 
Kuna wazee walinieleza walipewa kadi za kuwasaidia wazee kupata matibabu bure kwenye hospitali ya wilaya. Chaa ajabu wakifika kule wanawekwa kwenye bench lao, daktari anawaona baada ya waliolipa wote kumalizika, hiyo inakuwa saa kat ya saa saba na saa nane mchana. Dawa wanazoandikiwa sasa, hujamaliza kujieleza tayari prescription ina paracetamol. Wanaona ni kheri tu walipe wahudumiwe kama wengine.
Inasikitisha kwa kweli.
Huo ni ukatili kwa wazee wetu
 
Taratibu za rufaa hazifuatwi ndio maana wanachangishwa. Wanatikwa kuanzia zahanti ikishindikana anaenda kituo cha afya halafu ndio hospital za wilaya. Wafate huo mlolongo uone kama watachangia huduma ya afya
 
Back
Top Bottom