Wizara ya Afya na ARV Feki Nayo ni Siasa Chafu?

Nataka kujua elimu ya Dkt Lyimo na chuo alichosomea hana shule kabisa ya HIV/AIDS pia ARV inavyoonekana hajui nini hata madhara na zinavyofanyakazi hajui, na kama kweli ni daktari basi wagonjwa wetu wako hatarini.
 
Wakijiuzulu amtopata waziri na katibu kama wao ambao watawe kuingiza dawa bandia!
 
Kwa hali hii ya kuruhusu na kuachia dawa bandia ziingie nchini na kusababisha vifo na maafa kwa wananchi hawa mawaziri na kundi lake lazima wawajibishwe. Tukumbuke ni hivi karibuni ziliingizwa dawa za malaria fake na dawa nyingine nyingi. Rushwa uvivu na kutokupenda maisha ya wengine vinatuuwa sasa. Wito lazima wawajibike.

Daktari: Serikali inahusika ARV bandia Send to a friend
Monday, 24 September 2012 20:11

aids-arvs-vidonge.jpg
ATAKA IJIHOJI IJE NA MAJIBU, AELEZA ATHARI ZAKE, NAIBU WAZIRI ATAKA IPEWE MUDA ZAIDI KUCHUNGUZA TATIZO
Elias Msuya
WAKATI utata ukiendelea kugubika usambazwaji wa dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV), daktari katika Kitengo cha Ukimwi, Dar es Salaam ameitaka Serikali kujichunguza yenyewe, kwa kuwa dawa hizo hazisambazwi na watu binafsi.

Daktari huyo, Charles Lyimo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Dawa katika Kitengo cha Ukimwi Hospitali ya Amana, alisema jana kuwa hakuna sababu ya kutafuta mchawi kwenye tatizo hilo; Serikali inahusika.

"Siyo rahisi kujua kwamba hii ni dawa halisi au bandia, lakini tuna uhakika na dawa tunazotumia kwa sababu zinaagizwa na Serikali peke yake. Hakuna mtu binafsi aliyepewa tenda (zabuni) ya kuziagiza," alisema Dk Lyimo.
Dk Lyimo alisema awali, dawa hizo zilikuwa zikiagizwa kutoka Marekani, lakini baadaye utaratibu huo ukabadilishwa na zikaanza kuagizwa kutoka India.

"…(Serikali) inapeleka oda kiwandani na ndiyo inayozigawa dawa hizo na kuzisambaza kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Lakini pia dawa hizi zinatengenezwa Arusha kwenye kiwanda kilichopewa kibali na Serikali," alisema Lyimo na kuongeza:

"Kama kuna dawa bandia, basi Serikali ijihoji. Kwanza mimi ninaposikia habari hizo huwa nacheka tu kwa sababu tangu sakata hili limeanza, wizara inajigongagonga tu… hawatuhusishi wala kutuuliza… na sisi tunaendelea tu kugawa dawa…"

Alipotakiwa kueleza tofauti iliyopo kati ya ARV zinazotengenezwa India na zile za Tanzania, Dk Lyimo alisema: "Ni sawa na dawa za kutuliza maumivu za Panadol na Asprin. Kuna wagonjwa wenye vidonda vya tumbo hawawezi kutumia Asprin, hawa wanatumia Panadol. Vivyo hivyo kwenye Ukimwi kuna wagonjwa ambao wanapata madhara wanapotumia dawa za India. Hawa sasa tunawapa dawa za Tanzania."

Dk Lyimo alisema mgonjwa anabadilishiwa ARV kulingana na jinsi zinavyompenda au kumdhuru na ikifikia hapo, mgonjwa huyo anahitaji uangalizi wa karibu wa daktari.

"Kuna dawa zinazonyonya damu, nyingine zinakula nyama na nyingine zinaleta maruweruwe na njozi mbaya. Kwa hiyo tukiona athari hizo tunambadilishia mgonjwa dawa hizo," alisema Dk Lyimo.
Akizungumzia madai hayo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alikiri kuwa ni Serikali pekee inayoagiza dawa hizo kwa ajili ya wananchi wake na akataka jamii ifahamu pia kuwa ni Serikali hiyohiyo iliyogundua tatizo hilo na kuanza kulifanyia kazi.

"Ni kweli Serikali pekee ndiyo inayoagiza dawa na Serikali hiyohiyo ndiyo iliyounda TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa), ambayo kwa kazi nzuri imefanikiwa kugundua kuwapo kwa dawa bandia. Kwa hiyo tuwape muda wa uchunguzi," alisema.

Hata hivyo, hakusema itaichukua TFDA muda gani kumaliza kazi hiyo akisema: "Hii ni kazi ya kitaalamu na inayohusisha mambo mengi. Siyo kwamba muda haujulikani, ripoti hiyo bado iko kwenye uchunguzi na uchunguzi unachukua muda mrefu… Tuwape muda wataalamu."

Hata hivyo, mmiliki wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPIL) kinachotengeneza dawa hizo, Zarina Madabida alikaririwa na gazeti hili jana akisema kuwa ndicho kilichogundua kuwapo kwa dawa hizo na kutoa taarifa kwa TFDA kikiomba iingilie kati ili kuondoa dawa hizo bandia kwenye mzunguko.

Athari za ARV bandia
Kuhusu athari za dawa bandia, Dk Lyimo alisema mgonjwa anayezitumia hana tofauti na mtu anayekula unga ambao kimsingi hauwezi kutibu maradhi.

"Dawa bandia siyo lazima iwe na madhara kwa mgonjwa. Cha msingi hapo ni kwamba mgonjwa anayetumia ARV bandia anakuwa tu hajatumia dawa kwa muda unaotakiwa," alisema na kuongeza:

"Mtu anaweza kutumia tu unga kutengeneza vidonge kisha akaweka nembo kwenye makopo na kuziuza kama ARV, hii ni kuwalaghai wagonjwa."

"Mtu asipotumia dawa, kama CD4 zake zilikuwa zimeongezeka hadi kufikia 500, hushuka tena na wale wadudu hupata nguvu ya kushambulia vile virutubisho vya seli. Kwanza wadudu wale huwa wajanja zaidi na wanaweza kujibadilisha kama kinyonga. Hivyo mgonjwa hurudiwa na magonjwa nyemelezi… ni hatari mno."

Dk Lyimo alisema kwa wastani hupokea kati ya wagonjwa 250 hadi 300 kwa siku hospitalini hapo na wote huja kuchukua dawa ili kuendelea na dozi zao. Alisema kutokana na usugu wa wadudu hao na tabia yao ya kubadilika badilika, dawa hizo ziko katika mchanganyiko wa makundi matatu yanayotosha kupambana nao.

"Kwa kawaida mwanadamu akiwa mzima ana CD4 1,500. Lakini akiathiriwa na Ukimwi zinapungua kwa sababu wale wadudu wanapoingia hushambulia virutubisho (membrane) na seli za kinga ndani ya damu.

"Hujipenyeza kwenye seli hizo na kujibadilisha na kufanana na seli hizo na huko ndiko wanakozaliana. Mtu anapotumia ARV, huvilewesha virusi na kuvifanya vishindwe kuzaliana, hivyo hula na vikishiba vinalala tu, lakini havifi," alisema.

Alisema kutokana na gharama kubwa ya dawa hizo, wagonjwa hushauriwa kutumia ARV wakiwa na CD4 350, hata hivyo, wapo wanaoshindwa kuvumilia hasa kutokana na kuandamwa na magonjwa nyemelezi hata wanapokuwa na CD4 600.

Kweli Rais Mtarajiwa ajiuzulu ? Wewe Umeona JKT Imevunjwa sababu yake ? Leo hii unataka ajiuzulu ?
 
Madaktari walilalamika na kugoma, tukaishia kuwatukana matusi ya nguoni.

Dr. Mwinyi wewe ndiyo unafaa kuwa Waziri wa Afya kwa Taifa la Tanzania.

Mtu asikubabaishe wala kukutisha, endelea kupiga mzigo tu Mzenji wewe.

Kama hawa Watanzania hawajui kudai haki zao, Acha wafe.

Mchungaji Msigwa anasema "Asiyefanya kazi na asile......."

".....haki haiombwi ila inadaiwa." Kama sisi HATUTAKI kudai, wewe endelea tu na kazi.
 
Tanzania haina hata kiwanda kimoja wala wasomi wa kutengeneza dawa za ARV wametambuaje kwamba hizo dawa ni feki? What I know is that tbs and the mkemia mkuu are not conversant with the ingredients of ARV. Au kwa kuwa zimetokea India na sio US. Tangu lini mtoto wa standard II aka-moderate mtihani wa form VI?
Please be constructive here and you are required to think as a human. Don't polticize this; it is about life or death!!
 
This is the price we are paying for having Serikali dhaifu madarakani. Nadhani somo la umuhimu wa serikali limeeleweka zaidi kwa watanzania wakati huu wa awamu ya JK. Too bad ni kuwa vigogo wengi hawatumii hizi ARVs za 'bure' za serikali.
 
Haya madhara yatampata kila mtu maana yanatumika kulisha kuku na nguruwe na mifugo mingine. Tumekwisha!
 
Ni vyema ukafuatilia suala hili vizuri, medical store department yes, lakini kabla dawa hazijaingizwa ndani ya nchi ni lazima TFDA waidhinishe ubora wa dawa au chakula kwa maisha ya binadamu. Suala la usambazaji ni lingine kwa kuwa tayari zipo ndani ya nchi. Hata kama zimezalishwa ndani ya nchi bado TFDA bado wanarole ya ku-play usiwatete hapa. Narudia hapa hakana upelelezi unaohitajika zaidi ya watu kuwajibika kwa kuwa kila kitu kiko wazi hizi dawa hazikushuka kutoka juu bali zilipokelewa kutoka taasisi moja kwenda nyingine kwa utaratibu maalum na unaoeleweka.

Mkuu dawa ni ya TPI, TPI ni ya tanzania... zimeingizwa toka wapi? na unajua utaratibu wa kupokea dawa hadi zikafika kwenye inventory ya MSD??

Imported ni rahisi kwa counterfeit kwasababu zinatoka nje, na ni rahisi zaidi kama dawa zinauzwa, sasa hii ya public supply system tena ARVs ambazo haziuzwi bado unahoji??
 
lakini MSD hawezi kupima na kujua ufake wao si wanasambaza.
Kwani hawa TFDA wanajukumu gani kama sio kuhakikisha hatutumii vyakura au madawa fake?
inapimwa wakati gani na inasambazwa wakati gani??

na kama ni local product zinapimwa vipi na zinasambazwa vipi??

quality control ya madawa iko namna ka atatu wakati wa kutengeneza, wakati wa procurement na kupokea na post market....

waliogundua fakeness ni TFDA, waliokagua ni TFDA lakini ukaguzi unafanywa kwa kupata samples.... samples anatoa nanai?? supplier, in our case supplier ni nani?
 
Nilishasema, kuna siasa imeingia humo

TPI wanasema wamegundua dawa feki zinasambazwa.... na nani??? zilifikaje kwenye circulation?? ilikuaje wakagundua (wa mfumo wa follo-wp)??

Kuna watanzania wanafaidika na weka system, wanaiabuse, bahati mbaya kuna internationl organizations wanaofanya verification ya kila kitu.......... wale wa zamani wanambuka EMTRI, nani alichukuliwa hatua??? hakuna hata mmoja

NI DAWA FEKI AU DAWA ZILIZOFELI QUALITY CONTROL TEST NA ZIKAGUNDULIKA KUTOKANA NA INTERNATIONAL TESTS???

there is a huge difference between counterfeit and substandard product
 
hapa serikali inahusika moja kwa moja,tusihangaile kutafuta mchawi na wakati anajulikana kbs,Serikali ingekuwa makini mambo kama haya yasingekuwa yanatokea.
 

Dr. Hussein Ally Mwinyi, yupo katika uwaziri alionao kama fadhila ya Jakaya Kikwete kwa Mzee Ruksa, kwani yeye ndie aliemteua kuwa mkuu wa wilaya, baadae naibu waziri hadi waziri kamili. Kikwete anajua kulipa fadhila jamani......!

Tuje kwenye ARV feki.

Ipo hivi, ili uingize dawa au vipodozi hapa nchini ni upeleke INVOICE ya manufacture kwa TFDA. Wao (tfda) watazitambua hizo dawa au vipodozi, kisha watakutoza 1.5% ya FoB kama zinaruhiswa kuingia nchini.

Mzigo ukiingia hapa nchini (Dawa na Vipodozi), TFDA na TBS woote huja kwa ukaguzi...mara nyingi nimeshuhudia TFDA na TBS wakilumbana kuwa nani ana mamlaka ya kukagua na kuidhinisha kuingia kwa mzigo. Lakini TFDA hushinda pambano, kwani impoter huja na copy au risiti ya malipo aliyolipia. Kwa kuongezea ni kwamba, ili TFDA wakuruhusu pia uingize dawa ni lazima uwe na leseni ya pharmacy hapa nchini.

Wakati wa ukaguzi wa conteiner, TRA, TBS na TISS wanatoa afisa angalau mmoja kukagua container yeyote inayoingia hapa nchini.....! Halikadhalika kupitia airport, hali ni hiyohiyo kwa wakaguzi.

Swali, inawezekanaje kuingizwa kwa dawa hapa nchini bila vitengo hivyo kujua.......?

  • Dawa zimetoka kwa supplier gani ambao wao wanamtambua?
  • Kama mwingizaji dawa amezitoa kwa supplier mpya,nao wakaona wamruhusu aziingize, kwanini wasizipime kujua ubora wake?
  • Kila anayeingiza dawa, huwa dawa zake hurekodiwa batch number na TISS, TFDA, TRA na TBS....! Vipi waimtaje alieingiza na kumchukilia hatua?

Jibu ni moja kwamba, serikali inahusika moja kwa moja na uingizaji wa dawa hizi kwakua hakuna mfanyabiashara atakayeziingiza hizi dawa akaweza kuvuka wakaguzi wote hao halafu akaishia kuzigawa bure....kwakuwa haziuzwi. Wajanja wameziingiza kwenye mzunguko ili fedha za serikali na za wafadhili zinazogharamikai tiba hii ziingie mfukoni mwao katika kununua dawa feki za bei poa ili kutuulia ndugu zetu........!

Ulinzi na USALAMA oyeeeeeeeeeeeeeeeee!

Kibanga Msese
 
Back
Top Bottom