Wizara ya Afya kwanini mruhusu dawa za meno zenye Flouride ziuzwe na zitumike Tanzania?

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,885
28,246
Wakuu
Hua kuna vitu vidogo vidogo sana ambavyo mamlaka za serikali zikishirikuana wanaweza kuokoa maisha ya Watanzania.

TFDA na TBS wameshindwa kufahamu kua dawa za meno zenye content ya Flouride sio nzuri kiafya na ni sumu kali.

Je kwa nini msijifunze kwa mataifa ambayo dawa zao za meno ni marufuku kua na Flouride na Dawa ikiwa na Flouride ni For Export Only.

Wataalamu wetu sijui mnakwama wapi kwenye kulisaidia Taifa na Kuokoa nguvu kazi ya Taifa
 
Sitaki kutaja na sijaongelea kirefu zaidi lakini amini flouride sio nzuri kabisa kiafya
 
Many things you feared has been in your place for your (deleted peoples)
 
Dawa zisizo na fluoride naonaga kaka zimepoa sana hata hazisisimui.
 
Fluoride is a mineral that occurs naturally in water sources. Sometimes, additional fluoride may be added to a community's water because it has been shown to help prevent cavities. Fluoride makes teeth stronger and more resistant to cavity-forming acids, working to prevent decay long before you would even notice it AND If you have a child under the age of two, the child should definitely be using a fluoride-free toothpaste. According to the American Dental Association, a child can swallow too much fluoride, especially at the ages of two and under, when it's tough to teach them to spit out toothpaste. When too much fluoride is taken in, it can lead to dental fluorosis.This particular condition causes discoloration or pitting on the teeth. It may appear as brown spots, scattered white specks or white spots.Kwahiyo inaonekana si bora kwa watoto na sio kwa watu wazima...
 
Mkuu mleta mada tafadhali,umefanyia wapi huu utafiti wako kuhusu FLUORIDE? Maana hii fluoride inahitajika sana kwa binadamu kwa ajili ya kusaidia binadamu.

Fluoride hupatikana kwa asili katika udongo mfano waliochimba visima vya maji, kwenye maji ya kawaida, na hata kwenye baadhi ya vyakula. Pia hutolewa kiutaalam kwa matumizi ya maji ya kunywa, dawa ya meno, kuoshea kinywa na bidhaa mbalimbali za kemikali.
Mamlaka ya maji mfano DAWASCO wanaongeza fluoride katika usambazaji wa maji wa manispaa, kwa sababu tafiti zimeonyesha kuwa kuiongeza katika maeneo ambayo viwango vya fluoride katika maji ni chini kunaweza kupunguza kiwango cha kuenea au kaharibika/kuoza kwa jino kwa idadi kubwa ya watu.
Labda tuiweke hii mada yako hivi Fluoride inatakiwa lkn kwa kiasi.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea hapa

https://www.medicalnewstoday.com/articles/154164.php
 
mmmmm, hivi sio km fluoride ndio inatakiwa kwenye Meno ili kuzuia kuoza?
Note : anything too much is harmfull.
 
TFDA na TBS hata ukiuza sumu ukienda kuwahonga pesa watakupa na muhuri wao kabisa.
 
Mtaifa mengine ambayo yalikataza matumizi ya flouride kwenye matumizi ya madawa ni haya yafuatayo
Denmark, Germany, Finland , France, India, Israel, Hungary, Northern Ireland , Sweden, Czech Republic
 
Labda kwa kukusaidia tu unachokiona pale kwenye dawa ni Fluorine, ikiwa kwenye form ya sodium fluoride na si Fluoride halisi ambayo ndio huwa ni hatari...

Na kwa kukusaidia tu, ni kwamba baada ya kuondolewa ile negative charge kwa njia ya dissociation ndio tunapata fluorine ambayo iko salama zaidi, na labda tu ushawahi kusikia process inaitwa water fluoridation kwenye maji ni katika kuongeza kiwango cha sodium floride (fluorine) ili kuweza kupunguza kiwango cha fluoride katika maji ili maji yaweze kuwa salama kwa matumizi na kuweza kuepuka meno kuoza kama ndugu zangu wa singida na manyara maji yao huwa yanakiwango kikubwa cha fluoride hivyo kupelekea kuwa na mezo yenye rangirangi (dental fluorisis).

Na kiwango cha fluoride kinachoruhusiwa katika maiji ni 1ppm na kisizidi hapo. Nimekutana na uzi mwingine mleta uzi akilalamika kuhusu kiwango cha risasi (lead) katika suppliment aliyonunua kwa ajili ya kutengenezea chakula cha kuku ila ukiangalia ni tolerable level kabisa hasa kwa hao kuku maana hata wanyama wametofoutiana katika kuhimili kiwango cha lead katika vyakula vyao.

Na niwajuze tu hasa hizo mbogamboga mnazonunua na kula ndio zinakiwango kikubwa cha madini ya lead, hasa kwa maeneo mengi hapa jijini dar es salaam mboga nyingi zinalimwa pembezoni mwa barabara na hivyo nyingi huwa zinakuwa na kiwango kikubwa cha lead na hii ni kutokana na moshi unaotolewa na magari kuwa na kiwango cha lead ndani yake, na katika research yangu moja ndio nikagundua watu wanalishwa kiwango kikubwa cha lead kupitia mbogamboga, hivyo hitimisho ningewaasa ndugu zangu epukeni kununua mboga mboga zinazolimwa pembezo ni mwa barabara au kama uko na uhitaji sana ni vyema ukaanzisha bustani yako hapo nyumbani ili kuepukana na hii kasumba hii.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom