SoC01 Wizara ya Afya iweke hiari ya kujitolea viungo vya mwili kisheria baada ya kufariki

Stories of Change - 2021 Competition

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Kama kichwa cha habari kinavyosema ni wakati sasa kwa serikali yetu kupitia wizara ya Afya kuweka hiari ya kujitolea viungo vya mwili tena kisheria ili viweze kutolewa kwa wahitaji mara baada ya mmiliki wa mwili kufariki

Ni hivi serikali kupitia wizara ya afya ipeleke muswada bungeni wa kuruhusu watu wanaohitaji kujitolea viungo vyao (mfano figo, bandama, maini, moyo, bone marrow na N.K) baada ya kufariki wawe na uwezo wa kufanya hivyo kisheria ili punde tu baada ya kufariki viungo vyao vitolewe vikatumike kwa wengine,

Kuna Ndugu zetu wengi wanamatatizo ya viungo either vimekufa au vinakaribia kuharibika kabisa na wana matumaini ya kuishi lakini tatizo ni wapi watapata mbadala wa Viungo hivyo ili waweze kuishi kadri ya matumaini yao hakuna! Na mwisho wanaishia kuishi na Kufa kwa uchungu huku wakisononeka,

Wakati huyo anakaribia kufa kwa kukosa kiungo flani cha mwili pembeni kuna jirani yake mwingine anakufa kwa magonjwa yasiyoweza kuzuilika huku viungo vyake vikiwa vizima kabisa

Kwanini huyu anaekufa na viungo vikiwa vizima pengine kungekuwa na sheria angeweza kusaini na kujitolea punde tu baada ya kufa kiungo chake hicho kizima kitolewe kiende kikampe uhai na matumaini ya kuishi huyo mwingine ambaye ana uhitaji,

Ni vigumu kunielewa, na itakuwa vigumu pia ili jambo kueleweka katika jamii yetu kwa sababu wengi wetu tumejawa na uoga wa kifo

Tunawaza tufe na kutolewa organ zetu hiyo itakuaje? Kwenye Kifo hakuna maumivu na hakuna chochote kwa hiyo hakuna jambo utahisi, ni swala tu la serikari kutoa elimu kwa jamii yetu,

Unaweza kukataa kutoa organ kwa uoga, lakini unajua pia baada ya kifo Ukishazikwa kuna kuoza,hizo figo, maini, moyo, bone marrow unazoogopa kutoa zikawasaidie wengine baada ya kifo chako!.
Punde tu baada ya kufariki na kuzikwa, siku ya tatu baada ya tumbo lako kupasuka ndani ya kaburi nazo zitaoza na kuliwa na wadudu(funza) sasa mwisho maamuzi yanabaki kwako kujitolea viungo vikawasaidie wenye huitaji au kuacha vioze ndani ya kaburi

Faida ni Nyingi zaidi ndio maana tulio hai tunapaswa tutafakari haya.

-ukijitolea figo yako leo baada ya kufariki utamsaidia yule ambae amekata tamaa kabisa ya kuishi na atakuwa na matumaini badala ya kuacha kioze kaburini,

-ukijotolea bone marrow yako leo Baada ya kufariki utamsaidia ata yule mtoto mdogo anaesumbuliwa na kansa ya damu aweze kuishi na kutimiza ndoto zake, badala ya kuacha yakaozee kaburini n.K

Faida ni nyingi ila kubwa ni Kuokoa uhai wa mwingine ambae aliishia kukata tamaa ya kuishi tena.

Hii sheria inapaswa kupelekwa haraka bungeni tena ata kwa hati ya dharura na elimu itolewe kwa jamii ili sisi ambao tuko tayari tuweze kusaini ili miili yetu baada ya kufariki viungo itajika vitolewe vikasaidie wengine,

Binafsi niko tayari kusaini na kujitolea kutolewa viungo vyangu punde tu baada ya kufariki, niko tayari ata kushiriki kutoa elimu hii kwa wengine, jamii inayonizunguka na Nk.

Nitakuwa na furaha na nitakufa kwa amani kama nikijua baada ya kifo changu basi baadhi ya viungo vyangu vinaenda kusaidia uhai wa mwingine. NIKO TAYARI ATA SASA.


Cc Zero IQ
 
Naunga mkono hoja mtoa mada. Ila tahadhari ichukuliwe isije ikawa wauguzi wanamis-use hii chance.

Kwamba wababe wanakuja na vibunda vya noti za kutosha halafu wewe umeenda zako kucheki malaria wanakuzimisha kisa wanajua status yako ukiondoka watachukua spea gani mwilini mwako.
 
Naunga mkono hoja mtoa mada. Ila tahadhari ichukuliwe isije ikawa wauguzi wanamis-use hii chance.

Kwamba wanababe wanakuja na vibunda vya noti za kutosha halafu wewe umeenda zako kucheki malaria wanakuzimisha kisa wanajua status yako ukiondoka watachukia spea gani mwilini mwako.
Kwa mujibu wa mkataba wako mkuu, ikiwekwa na Sheria kutakuwa na jinsi ya kudhibiti hayo pia
 
Mimi nilikuwa naomba karatasi fulani ni kitambulisho kwenye kuna kipengele kinauliza iwapo ukifa wachukue kiungo nikaweka hapana nikasaini.
 
Back
Top Bottom