Wizara ya Afya inatakiwa kuupitia upya muundo wa Uongozi

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
3,608
4,091
Naandika haya kwasababu imekuwa kama uongozi wa wizara hauyaoni. Angalia Mifano ifuatayo
1. Kuna Wizara ambayo kwa sasa inasimamia Hospitali za rufaa za kanda, hospitali za rufaa za mikoa na hospitali ya Taifa Muhimbili. Lakini pia kuna TAMISEMI ambayo husimamia hospitali zote za Wilaya na vituo vyote vya afya na zahanati.
2. Pia kuna team za uongozi/usimamizi wa huduma za Afya Mkoa (RHMT) na Wilaya au halmashauri (CHMT) na kuna uongozi wa Hospitali (HMT)

Changamoto inakuja kuwa hivi
Kwenye team za usimamizi wa afya mkoa/wilaya hapo ndio kuna changamoto kubwa sana

-Utakuta Mratibu wa Shughuli fulani mfano labda 'Malaria, Ukimwi, Kifua kikuu' mkoa ana advanced diploma (AMO), au chini ya hapo
-Pia utakuta msimamizi wa kitengo mkoa kama vile Maabara (RLT), Pharmacy (RPharm), Nursing (RNO), RSWO, RHO na wengine wana elimu ndogo kama vile diploma.

-Then unaenda kwenye halmashauri ambazo kimsingi zinatakiwa zisimamiwe na Team ya mkoa wana elimu kubwa sana, wengine unakuta wana BSc, MSc n.k

Linapokuja suala la Usimamizi shirikishi aliyepo mkoani anatakiwa aende wilayani akampe ujuzi huyo aliyeko wilayani, hapo ndio kizaazaa kinapokuja.

1. Utampaje technique aliyekuzidi elimu na ujuzi?
2. Mara nyingine unakuta mratibu wa malaria ni afisa afya anaenda kumsimamia vipi huduma za malaria mtaalam either clinician au Laboratory scientists aliyepo wilayani.
3. Au aliyepo wilayani anaenda kum-supervise aliyepo kituoni mwenye professional yake. Yaani hizo team zimeundwa kimagumashi tuuuu na majungu majungu tuuuuu

Mfano aliyepo mkoani atapiga majungu ili aliyepo wilayani abaki hivyo hivyo na aonekane hafai kabisa lakini anapoenda kwenye usimamizi anamkwepa maana anakuwa anajua hawezi kum-supervise.

Ujinga...

Wizara na TAMISEMI wote hawalioni hili, bali wanabaki kujadili kuwa wizara na TAMISEMI kwa ujumla kuna mafunzo mengi lakini matokeo ni kidogo sana tofauti na resources na juhudi zilizowekwa ili kuboresha huduma.

Kifupi ni kwamba SEMINA NA MAFUNZO wanapatiwa watu wasiosahihi.

Kila mtaalamu afanye kwa level yake hapo ndipo mtakapoona mabadiliko la sivyo, tutaendelea kubaki nyuma tu.

Inatia hasira sana yaani mtu amesoma mazingira alafu anakuja kumfundisha au kumsimamia mtaalam wa diagnosis kufanya diagnosis very shame.

Alafu serikali wanasema wanataka mabadiliko chanya haitawezekana

Fanyeni reform angalieni huyu yupo hapo je hakuna watu wenye fani husika au wenye ujuzi mkubwa??????

Huu uzi usiunganishwe naomba nipate mawazo tofauti inawezekana ni mawazo yangu potofu labda wizara inamalengo yake.
 
Kuna ka ukweli kwa mbaaali kidogo lakini umesahau kuwa hivyo vyeo ni vya kiutawala na uzoefu zaidi na havizingatii utaalamu wa kubobea mbali na semina za hapa na pale, kwa mfano Waziri wako wa Afya ni mwanasheria lakini ana head wizara ya Afya bila kuleta matatizo makubwa ya kitaalamu, na kw a upande wa pili hawa uliowataja mara nyingi ndio huwapokea hao wasomi wako na ndio wao huhakikisha kuwa wanakupangia kazi mbali na ofisi zao ili usije kupokonya nafasi zao na linapokuja swala la recommendation hapo ndipo vijana wanapomalizwa kwani majamaa ni wajuzi wa majungu na fitina za kila aina
 
Sasa hapo chief si ndipo unaona majungu yanapoanzia. Kikubwa hapo ni Technique sio uzoefu, yaani wao ni full majungu na kujipendekeza kwa wakubwa.
 
Kuna ka ukweli kwa mbaaali kidogo lakini umesahau kuwa hivyo vyeo ni vya kiutawala na uzoefu zaidi na havizingatii utaalamu wa kubobea mbali na semina za hapa na pale, kwa mfano Waziri wako wa Afya ni mwanasheria lakini ana head wizara ya Afya bila kuleta matatizo makubwa ya kitaalamu, na kw a upande wa pili hawa uliowataja mara nyingi ndio huwapokea hao wasomi wako na ndio wao huhakikisha kuwa wanakupangia kazi mbali na ofisi zao ili usije kupokonya nafasi zao na linapokuja swala la recommendation hapo ndipo vijana wanapomalizwa kwani majamaa ni wajuzi wa majungu na fitina za kila aina
Scrap 100%
 
Bandiko lako linaonesha umejawa na hasira kali mno,plus uchu wa kutaka kuwa Boss na majivuno ya elimu kubwa uliyonayo.

Kwa kukusaidia tu TAMISEMI ilishatoa waraka wa maelekezo kwa Mikoa kuhakikisha kuwa wale wanaoitwa " wenye elimu" kubwa ndio wapewe nafasi za uongozi,na utekelezaji wake umeshaanza kufanyika.

Pole kwa maumivu,kuwa mpole utapewa cheo na weye.
 
Kuzunguka kote ulitaka kuongelea semina, kuhusu usimamizi shirikishi (Supportive supervision) unazopatiwa na waratibu sidhani kama zinakua zinaingilia utaalamu hasa pale anaekusimamia akiwa hana elimu ya hicho kitu ama elimu ndogo, zaidi anachotakiwa kufanya ni kukueleza kwa kuzingatia miongozo na kuona kama unaifuata miongozo hiyo. Lakini pia kwenye point yako ya kwanza umeongea kishule zaidi na sio kwa kuzingatia hali halisi iliyopo maeneo ya kazi. Unafahamu kwamba kuna MO wanaositisha kufanya upasuaji na kuagiza kuitwa kwa watu wenye uzoefu hasa AMO pale wanapokutana na changamoto huko ndani? Unajua kwamba kuna Medical Attendants wenye skills kubwa za kufanya kazi kuliko MO’s wengi japo wanakosa maelezo ya kitaalamu kwanini wanafanya hivyo vitu kwasababu hawaijui Physiology wala Pathology!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom