Wizara ya afya! Huu ni wakati wa kutekeleza ilani ya CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya afya! Huu ni wakati wa kutekeleza ilani ya CHADEMA!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ziroseventytwo, Sep 26, 2012.

 1. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,555
  Likes Received: 1,556
  Trophy Points: 280
  Ndg zangu wanaJF, leo nilikuwa naangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku kituo cha ITV, nikamwona mama m1 wa kibamba anayesumbuliwa na tatizo la kuvimba mguu. Tatizo lake limemsabishia madhila makubwa sana, pamoja na kusaidiwa kila kitu anapata maumivu makali sana. Kwa mujibu wa mama huyo, mume wake na mama yake mzazi zinatakiwa kiasi cha dola 20000 za kimarekani kwa ajili ya matibabu yake nchini india. Na mpaka sasa wana 3.5 hivi Tsh. Bado kama 27000000/=hivi kufanikisha zoezi la matibabu kwa mama huyo. Hapa ndo panapoitajika utekelezaji wa ilani ya chama cha CHADEMA hususani kwenye sekta ya afya. Ukisoma ilani ya cdm kwenye sekta ya afya (kama ntakuwa nimeelewa)inasema wazi, kutakuwa na bima ya afya kwa kila mtanzania. Siyo kwa hiyari. Ni lazima. Akiifafanua, Mabere Marando alisema kila mtu anapaswa kuchangia angaloa 15000-25000 kulingana na kipato cha mtu. Leo hii CDM wangekuwa madarakani, kwa mujibu wa ilani yao,kupitia mfuko huu wa bima ya afya mama huyu angekuwa anapata matibabu kwa wakati,tiba bora kwa kutumia kiasi kidogo tu cha mchango wake kwenye bima ya afya. Wakati umewadia sasa, kuacha kutumia mipango mizuri, hata kama ni kutoka upinzani. Ccm kupitia wizara ya afya wasisite kulichukua hili kutoka CDM kwani lina manufaa kwa umma wa watanzania. Nawasilisha.
   
Loading...