#COVID19 Wizara ya Afya hamtutendei haki, kipimo cha COVID19 ni ghali sana

Mnyakyusa Ipinda

JF-Expert Member
Dec 9, 2020
439
1,526
Kwako waziri wetu wa Afya Dr. Gwajima.

Sijajua sababu ilofanya hadi muweke bei ghari hivyo kuoata hichi kipimo kwa wanaosafiri, kipimo ni 235,000 Tsh. (100 USD) , hii sio sawa kiukweli mnatuumiza sana sisi wa vipato vya chini ambao tunapata visafari vya dharula katika kutafuta maisha, huu ni unyonyaji, mala ya mwisho ilikua ni elf 40 kupima na ilikuwa very fair, sijajua why mmefanya kiwe ghari, alafu kibaya zaidi hamuweki taarifa wazi, yani mtu hadi uende maabara ya Taifa ndo unaambiwa.

Haya pili kumbe mmehamishia upimaji wa Covid kwenye Hospitali zingine na maabara ya taifa imebakiza kupokea samouli tu, lakini hakuna taarifa zozote kwa umma (unless sikuona mimi) ila nilikuta watu wengi wanaenda mabara ya Taifa wanaishia getini wanaambiwa sasa hivi hawapimi. Mnatukosea jamani, yani Wizara ya afya mambo mengi hayako wazi na yaliyoko wazi hayako sahihi, huku mnasema hivi mtu akienda hospitalini au taasisi zilizo chini ya wizara anakuta mambo tofauti, hii sio sawa kabisa.

Waziri Gwajima wewe ndo waziri wa sasa na unajitahidi sana lakini hili la kipimo cha Covid hapana jamani msifanye kama ndio kitegauchumi mtakua mnatuumiza, sio kila anaeenda nnje ya nchi ana uwezo, wengine ni waganga njaa tu, au hata wale tunaosafiri East Africa basi mngeangalia upya bei za kupima, kaeni na wadau muone mnatusaidiaje wananchi wenu.

Hapa nimeandika kwa hudhuni sanan sababu nahisi nakosa interview yangu ya kazi sababu sina uwezo na nimepata kazi Uganda huko na natakiwa nisafiri, nimejichanga kwa ndugu jamaa na marafiki ila la Covid nimeshindwa na sijui nafanyaje manake nimeenda hadi Maabara ya Taifa kupeleka ombi langu nisaidiw nipimwe ili niwahi kazi wamekataa wanasema kipimo hakina exemption , 😭😭😭 Kama mkulugenzi upo humu unisikie , hii sio sawa jamani. Nakosa hata cha kuandika sababu nimeghafirika na sijui la kufanya, yani budget yangu nzima ya kwenda na kurudi na kuishi huko ndio bei ya kupima Covid....
 
POLE SANA. SERIKALI YA TANZANIA INGEKUWA NA NIA NJEMA YA KUPAMBANA NA CORONAVIRUS INGEFANYA UPIMAJI BURE KAMA ILIVYO MATAIFA MENGINE.
Yani wanakwaza sana, sasa hapo sijajua hata alotoa hiyo bei elekezi alitumia vigezo gani, yani bado kuna mtu anaamini kwamba kila anaeenda nnje ya nchi ana uwezo, na kwa nini iwe ghari hivyo , kuna watanzania wengi tu wa kipato cha chini wandugu zao Mombasa, Nairobi , Uganda, Rwanda, sasa hata msiba ukitokea ghafla au fursa watu watashindwa sababu ya ughali wa kipimo, usafiri mtu utapanda mabasi utafika kwa bei ndogo tu, lakini kipimo kinazidi hadi gharama za usafiri kweli? Sio sawa kabisa sio sawa
 
Yani wanakwaza sana, sasa hapo sijajua hata alotoa hiyo bei elekezi alitumia vigezo gani, yani bado kuna mtu anaamini kwamba kila anaeenda nnje ya nchi ana uwezo, na kwa nini iwe ghari hivyo , kuna watanzania wengi tu wa kipato cha chini wandugu zao Mombasa, Nairobi , Uganda, Rwanda, sasa hata msiba ukitokea ghafla au fursa watu watashindwa sababu ya ughali wa kipimo, usafiri mtu utapanda mabasi utafika kwa bei ndogo tu, lakini kipimo kinazidi hadi gharama za usafiri kweli? Sio sawa kabisa sio sawa
Siku moja nilimsikia waziri akijitetea eti na wao huko wanauziwa bei kubwa!!nikajiuliza ina maana hizo nchi tena za kiafrika zinazopima watu wake bure, wao wanavitengeneza?!!shida ni pale serikali inataka kufanya biashara badala ya huduma!!kama mask tu tayari wameshaanza kuziuza kuna nini hapo?!nani mwenye kulusemea hili?!!
 
.... visafari vya darula .....mala ya mwisho .....alafu kibaya zaidi
... nimeandika kwa hudhuni... .....Kama mkulugenzi upo humu....
Mkurugenzi. Sio mkulugenzi

Mara ya mwisho. Sio mala ya mwisho

Huzuni. Sio hudhuni.

Dharura. Sio dharula.

Halafu. Sio alafu.

Bora usiende kwenye huo usaili, ungepoteza nauli na tozo ya kipimo. Hujui kuandika Kiswahili, utaweza nini, kupikia chai maofisa?
 
Mkurugenzi. Sio mkulugenzi

Mara ya mwisho. Sio mala ya mwisho

Huzuni. Sio hudhuni.

Darura. Sio dharula.

Halafu. Sio alafu.

Bora usiende kwenye huo usaili, ungepoteza nauli na tozo ya kipimo. Hujui kuandika Kiswahili, utaweza nini, kupikia chai maofisa?
walimu wa kiswahili sijui walifeli wapi...hili ni janga la kitaifa
 
Mkurugenzi. Sio mkulugenzi

Mara ya mwisho. Sio mala ya mwisho

Huzuni. Sio hudhuni.

Halafu. Sio alafu.

Bora usiende kwenye huo usaili, ungepoteza nauli. Hujui kuandika Kiswahili, utaweza nini, kupikia chai maofisa?
Ungeweza kurekebisha tu bila kejeli zako, hii sio mada ya kujifunza lugha ya kiswahili ndugu, i hate this kind/level of stupidity , watu wanaleta thread zao badala ya kurekebisha tu palipokosewa mtu unaanza kukejeli as if you are perfect in everything.
 
Hivi hamuelewi kwa hzo bei ni kwamba hamtakiwi kupima na ukienda kupima majibu lazima yaje negative.Tanzania hakuna corona.
 
Hivi hamuelewi kwa hzo bei ni kwamba hamtakiwi kupima na ukienda kupima majibu lazima yaje negative.Tanzania hakuna corona.
Hata kama wanahisi hakuna korona lakini hilo ni hitaji la kimataifa, huwezi kuingia nchi nyingine bila hiyo document, kama ni hivo wasitupime watupe tu hayo madocument tusafiri, kama hakuna tunapima nini sasa tena kwa gharama yote hiyo. Ni hatari sana
 
Kwa masikitiko makubwa, unalipa dola 100 una fanya booking ya kupima unafika kituon unaambiwa hapa hatupimi covid, wakati wakiweka ivyo vituo sikujua kusudio lao ni nini..Hii imenitokea mm,nimejichanga nkalipa dola 100, nkabook mnazi mmoja,nafika naambiwa hawapimi niende Amana,nafika Amana natakiwa tena kulipa 25 elfu nlichoka.

Haiishi hapo,unaambiwa utatumiwa majibu unasubri 48hrs hakna majibu mpaka uwapigie simu wa kuhoji ndo wakupe majibu..Ilifika sehemu nkaanza kuchukia viongozi bila sababu
 
Back
Top Bottom