Wizara ya Afya: Hakuna tishio la UVIKO-19, likiwepo tutatoa taarifa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Wakati Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) likiwataka waumini wake kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya corona ambavyo vimeshambulia nchi kadhaa, Serikali imewataka wananchi kutoingiwa na hofu bali wasubiri maelekezo ya Serikali.

Waraka wa tahadhari wa TEC ulitolewa jana na Rais wa Baraza hilo, Gervas Nyaisonga akiwaandikia Kardinali, maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wastaafu ikiwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Tahadhari juu ya maambukizi mapya ya virusi wa korona na ugonjwa wa Uviko-19 (covid-19)”

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi jana, Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto, Dk Goodluck Mollel alisisitiza msimamo wa Serikali kuwa hakuna tishio la ugonjwa wa Covid-19 na likitokea watatoa taarifa.

Katika waraka huo, Askofu Nyaisonga alisema tangu mwaka 2020 kumekuwa na hatua za kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona na zilizoonekana kufanikiwa.

“Kwa mwaka jana nchi yetu ilifanikiwa katika mapambano haya dhidi ya corona. Visa vya maambukizi ya corona vilipungua na baadaye tukaamini tumeshinda,” alisema Nyaisonga katika waraka huo.

Hata hivyo, alieleza mwaka huu kumekuwa na wimbi jipya la maambukizi ya corona duniani.

“Nchi kadhaa zimethibitisha kuwa zinapitia kwenye kipindi kigumu cha kuenea kwa corona na kutokea kwa vifo vya watu. Nchi yetu sio kisiwa,” alisema Askofu huyo.

Aliendelea; “Kwa uhalisia huo, tusiache kuwashauri, kuwahimiza na kuwaongoza taifa la Mungu katika mapambano haya dhidi ya virusi vya corona. Tuhimize mapambano dhidi ya virusi vya corona kwa kutumia silaha zote za kiroho, kimwili, kisayansi na za kijamii. Tusikome kuhimiza sala, kuepuka kugusana, kunawa na kujitakasa kila wakati, kuchukua hatua tuonapo dalili za ugonjwa na kuepuka misongamano hatarishi.”

Akizungumzia barua hiyo, Katibu Mkuu wa TEC, Dk Charles Kitima alikiri barua hiyo kuwa ya Kanisa Katoliki, akisema jukumu la kanisa ni kushughulikia uhai wa watu. “Moja kati ya majukumu ya Kanisa ni kushughulikia uhai wa watu. Serikali labda na vyombo vingine bado vinafanya utafiti na uchunguzi, lakini sisi tunaona watu wanaingiliana na nchi yetu iko huru, kwani watu wanaingia na kutoka nje, yanaweza yakatokea, wanaokuja wakatuletea.

Alipoulizwa kuhusu msimamo wa Serikali kuhusu ugonjwa huo, Dk Kitima alisema; “Serikali yetu itasema, lakini ukienda `airport’ (uwanja wa ndege) Dar es Salaam kuna watu wanaingia kutoka nchi zenye corona. Kwa hiyo sisi siyo kisiwa tunaishi na watu na wengine ni wagonjwa.”

Kauli ya Serikali
Akizungumzia tamko hilo, Dk Mollel alisisitiza hakuna maambukizi ya ugonjwa huo nchini, akawataka wananchi wasubiri maelekezo ya Serikali.

“Hamna kitu kama hicho. Hizo habari mnazosema ni za mitandaoni tu, tuwaachie wanasayansi wafanye kazi zao, subirini Serikali kama kuna tatizo itawaambia. Kwa sasa endeleeni na shughuli zenu kama kawaida,” alisema Dk Mollel alipozungumza kwa simu na mwandishi wa habari hizi.

Alisema suala la kuchukua tahadhari kama kunawa mikono kama wakati wa corona, haimaanishi kwamba corona imerudi.

“Hilo suala lilikuwa linasaidia mambo mengi zaidi ya corona. Sasa hao wanaosema tujikinge na corona ukiwauliza wamepima wapi wakathibitisha kwamba kuna corona, hawawezi kukwambia zaidi ya kusema kuna watu wanaobanwa na kifua. “Waulize, ni leo Watanzania wameanza kubanwa na kifua au ni kwa sababu mvua imeanza? Kwani nimonia imeanza leo?

Tangu umezaliwa si umekuwa ukiambiwa watu wanaumwa kifua wakati wa baridi? Wakati wa baridi na wakati wa joto ni upi kuna kuwa na matatizo ya kifua? “ alihoji. Alipoulizwa kuhusu tahadhari zinazochukuliwa kwenye hospitali za Serikali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili ya watu kuvaa barakoa kwa wanaoingia, Dk Mollel alisema ni utaratibu wa kawaida.

“Kuingia na barakoa hata mimi ninapokuwa natibu wagonjwa natakiwa niingie na barakoa. Ni kitu ambacho kinatakiwa kifanyike, kwani hospitalini kuna magonjwa hayatakiwi yavaliwe barakoa?”
 
Nadhani majibu ya msaada yangekuwa kwanini wimbi la ubanaji kifua limezidi na wananchi wachukue tahadhari zipi kuhusu hilo wimbi sio waendelee na shughuli zao mpaka serikali itakapowaarifu.

Sasa ambao wapo katika kubanwa / mbioni kubanwa kweli hii statement inawasaidia ? Pili hata kama sisi hatuna wenzetu wanao si ingekuwa busara kuwaambia wananchi wasichukulie poa (jirani yako kama nyumba yake inaungua nadhani na wewe ni vema ukawa alert)
 
Kusema hakuna corona na wageni wanatiririka kila kukicha kutoka nchi zinazoathirika itakuwa jambo la kufikirika
 
Safari imejaa kila aina ya mawimbi na dhoruba ila nahodha anasema safari ni shwari, wasemao mawimbi na dhoruba hawakuona dhoruba ya mwaka jana... 😷😷😷
 
Mimi nadhani inawezekana akawa sawa, wimbi linaonyesha wanaume wazee ndo tumesikia wengi wanatutoka mimi nachoona ni magonjwa ya uzeeni Sasa kwa vile Kuna habari ya gonjwa mtu ugonjwa wake ukitibu tu anakuwa na mawazo yanayopelekea presha kupanda na mshituko.

Nacho shauri kwa vijana wa kiume muache kujifanya mamwinyi mbadilike kabisa ukiwa nyumbani jishughulishe hata kufua na kupasi nguo zako usitake kuhudumiwa Kama mgonjwa wakati ni huna tatizo yaani ukifika uzeeni utakuwa mchangamfu na kujiepusha na magonjwa ya uzeeni na damu itakuwa inachemka lakini hiyo tabia ya kusubiri Kila kitu mfanyiwe ndo sukari na presha zitazidi kuleta shida.
 
Back
Top Bottom