Wizara ya afya; Futeni gharama za kuchukua maiti mochwari katika hospitali za Serikali

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Ndugu zangu; kupanga ni kuchagua,
Nina imani na Ummy mwalimu atalifikisha hili kwenye cabinet!
angalieni uwezekano Wa kufuta gharama zote za
maiti kutoka katika hospitali za serikali! zikiwemo gharama za matibabu na huduma za mochwari!

Tuangalie namna nyingine ya kufidia pesa hizo!

Kama ELIMU Bure imewezekana sidhani kama hili litashindikana.

Zipo familia zinauguza kwa kuuza kila kitu hadi senti ya mwisho, bado mgonjwa anapofariki hupata wakati mgumu sana kukomboa maiti zao!

Viongozi Tuna dhamana ya kuwafariji wananchi hawa kwa kuwaondolea gharama!

UKISHINDWA KUTOA HUDUMA BORA BASI TOA JAPO HURUMA BORA!!!

Updates

Waziri wa Afya UMMY MWALIM leo Feb 14/2020; katoa maelezekezo hosp wasizuie maiti, watafte mbinu nyingine ya kudai pesa zao!

Note; Ni vyema kauli hii ili isipuuzwe na watendaji ingependeza kwa katibu mkuu wizara afya apeleke maelekezo hayo kwa maandishi hospitalini vinginevyo hayatatekelezwa kama hospitali hazitapokea order na mwongozo wa namna ya kufuta deni hilo! Maana watendaji wataogopa kuambiwa wamependelea au wamekula pesa

MAONI YANGU KAMA HAWAWEZI KUFUTA KABISA BASI WAFANYE HIVI

Kama wameshindwa kabisa kulifuta deni hilo! Basi hosipitali kupitia kitengo cha malipo ambapo kuna wakala wa bank ya NMB na CRDB; Kuwekwe utaratibu rahisi wa benki hizo kumlipia maiti kwa mkopo wa haraka (Instant mortuary loan)
kuwepo na fomu maalum inayotakiwa kujazwa na wadhamini /ndugu wa maiti, wakiambatanisha vitambulisho na barua toka serikali ya mtaa wanakoishi iwatambue ili waahidi ni lini pesa ile italipwa kwenye mabenki hayo bila riba ( faida ya mabenki itoke kwenye hospitali kwa wao kulipia kwa punguzo la asilimia 20% ya deni ili wao kama benki watakapokuwa wanadai mdhamini atawalipa pesa yote waliyodaiwa hospitali)!!
WANAWEZA KUBORESHA KAMA ITAWAFAA

AKSANTE
Screenshot_20200215-024353.png
 
Huduma za afya ni lazima ugharamie sasa ikiwa bure hospital zitashindwa kujiendesha sema wapunguze gharama au serikali itoe huduma ya bima kwa wananchi kwa gharama nafuu.
 
Huduma za afya ni lazima ugharamie sasa ikiwa bure hospital zitashindwa kujiendesha sema wapunguze gharama au serikali itoe huduma ya bima kwa wananchi kwa gharama nafuu.
Vipi kuhusu elimu, mbona serikali imesema ni bure bila kuhofia kuwa shule zitashindwa kujiendesha?

Kumbuka mleta maada amesema serikali iingaliwe namna nyingine ya kufidia gharama hizo.
Naona wazo la mleta maada ni zuri.
 
Hyo bure ni wanasiasa tu wanajikweza shule za serikaki zina hali mbaya tu watoto hata chakula hamna, paper zakufanyia mitihani shida, ndo mana wanafeli sasa hapo utalinganisha na Feza wanakolipa ada. Bure ni costful na sasa hivi ni ubepari huna fedha huduma za afya hupati.
 
We we mapato ya serikali yatatoka wapi?
Kuna mpango watu wenye Comments nyingi JF kulipishwa Kwa comment unalipa 50, sembuse mortuary
unamaanisha wanaokufa ndio wengi hadi wategemewe kutunisha mfuko?
 
Huduma za afya ni lazima ugharamie sasa ikiwa bure hospital zitashindwa kujiendesha sema wapunguze gharama au serikali itoe huduma ya bima kwa wananchi kwa gharama nafuu.
matibabu sawa! lakini hata kuchukua maiti mochwari napo gharama itahitajivbima?
 
Vipi kuhusu elimu, mbona serikali imesema ni bure bila kuhofia kuwa shule zitashindwa kujiendesha?

Kumbuka mleta maada amesema serikali iingaliwe namna nyingine ya kufidia gharama hizo.
Naona wazo la mleta maada ni zuri.
zipo njia nyingi tu tunaweza kuzitumia kufidia hiyo gharama! ikumbukwe hayo matukio ya msiba ni ya ghafla
 
Naona wadau baadhi hawajamuelewa mleta mada! Hajasema watu wote watibiwe bure bali ikitokea bahati mbaya mgonjwa kafariki basi kuna haja ya kuonesha huruma kwa wafiwa mfano kupunguza gharama ya kuchukua maiti mochwari kama sio kuondoa gharama kabisa!
 
kabisa Mkuu! ifike mahala tusiwe watu Wa kusahau machungu ya msiba, hayo matukio yapo na yanaumiza sana watu, ukute wameuguza mda halafu they end up disappointed! bado kuchukua mait wadaiwe pesa! ni bora tutafte njia nyingine kufidia
 
Watanzania tunapenda bure itafika wakati tutaitaka serikali itowe chakula cha bure kila familia kwa siku. Kwani hayo majokofu ya kuwekea maiti yalipatikana bure? Hao madaktari wanajitolea bure? Hilo jengo la hospitali limejengwa bure?. Utasema kodi za wananchi au sio? Kwani hata benki hutowa mkopo kwa hela isio yake lakini ukirejesha wanataka riba yao. Hakuna cha bure dunia hii kama huna hela ya maiti choma moto tu kama mabaniani, tumewachoka wapenda bure.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Ndukiiiii ‍♂️‍♂️‍♂️
Labda tujiulize ni pesa kiasi gani hutolewa na serikali kwenye misiba mikubwa kwa ajili ya rambi rambi,, je kuna tofauti kubwa na hili??
 
wengi tu! kama MV Nyerere waliweza kutoa million of money kufariji, hata huko hosp machungu ya msiba ni yaleyale watafte namna nyingine kucover
Credit! Uko sawa mkuu HURUMA inahitajika mda mwingine
 
Watanzania tunapenda bure itafika wakati tutaitaka serikali itowe chakula cha bure kila familia kwa siku. Kwani hayo majokofu ya kuwekea maiti yalipatikana bure? Hao madaktari wanajitolea bure? Hilo jengo la hospitali limejengwa bure?. Utasema kodi za wananchi au sio? Kwani hata benki hutowa mkopo kwa hela isio yake lakini ukirejesha wanataka riba yao. Hakuna cha bure dunia hii kama huna hela ya maiti choma moto tu kama mabaniani, tumewachoka wapenda bure.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Unamtoza nani? ikumbukwe unaowatoza sio hao waliolala kwenye hayo majoko
fu, nina chokisema ni kwamba kwasababu aliyekufa katoweka basi iangaliwe namna ya kumsamehe, tunawasamehe marehemu kwa niaba ya ndugu zake wapewe mwili Bure
 
Huduma za afya ni lazima ugharamie sasa ikiwa bure hospital zitashindwa kujiendesha sema wapunguze gharama au serikali itoe huduma ya bima kwa wananchi kwa gharama nafuu.

Mtoa mada amesema huduma za mochwari, kuna haja ya kumwangalia mtu tu na kujua huyu hawezi kulipa, acha kabisa mtoa mada amesema jambo kubwa kuna watu wanauza kila kitu hadi mwisho hawana kitu.
 
Back
Top Bottom