tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 22,962
- 20,388
Suala la serikali kuingiza udini kwenye elimu limepigiwa kelele kila kona. Kuna baadhi ya wadau wanaamini kwamba hata kabla hizi tahasusi za dini kuanza kufanya kazi, kuna uwezekano serikali ikazifutilia mbali kwani utekelezaji wa hizi tahasusi tayari umeishaanza kuleta mkanganyiko miongoni mwa wanajamii wakitaka hizi tahasusi zifutiliwe mbali kwani serikali haina dini na haipaswi kuendekeza mambo ya udini hadi kuyaingiza kwenye mitaala ya elimu.
Wakati vumbi la sintofahamu kuhusu sakata hili halijatua, mdau mmoja wa elimu ametoa ufafanuzi ufuatao na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania wapenda amani wasiopenda kuchanganya dini na masuala ya elimu. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa chini:
MAONI YANGU
Namuuunga mkono huyu mwanazuoni 100% na naitaka serikali ifutilie mbali huu upuuzi kwenye mitaala ya elimu kwani unaweza kuligawa taifa pakubwa. Wewe fikiria dini ya asili na dini ya kihindu imeachwa bila kuingizwa kwenye mtaala unadhani wapagani na wahindu wataielewa serikali kwa kuwabagua kuwadharau kiasi hiki?
Pia tukumbuke hata wakristo na waislamu wamegawanyika sana. Yaani hili suala la udini litaleta mgawanyiko mkubwa sana katika taifa hili ikiwa hii serikal ya kusadikika itaendelea na msimamo wake wa kuingiza udini kwenye elimu.
Sasa hivi kila dhehebu lina biblia yake. Waumini wa Shia wana korani yao na waumini wa Ahmadiya wana korani yao pia. Aidha, korani zinazotumika Zanzibar ni tofauti na hizi zinazotumika hapa Tanganyika. Je, ni biblia au korani ipi itatumika kufundishia? Na je, itakuwa korani ya Zanzibar au ya Tanganyika? Kwa vyoyote vile serikali imefanya jambo la kipumbavu sana kuchomekea udini kwenye taaluma. Naomba wizara ya elimu iangalie upya hili suala kabla halijaigawa nchi vipande vipande.
Nawasilisha.