Wizara: Ni sahihi kuchoma vifaranga na utaratibu unatambulika kimataifa, yarusha lawama kwa waliosambaza picha

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,426
7,736
Wizara ya mifugo na uvuvi imetetea uamuzi wa kuchoma vifaranga kwani ni utaratibu unaotambulika kimataifa na kwa mujibu wa sheria namba 17 ya sheria ya wanyama ya mwaka 2003 imechukua uamuzi huo wa kuteketeza vifaranga hivyo 6400 ili kuepusha kusambaza mafua ya ndege.

Msimamo huo umetolewa na katibu mkuu wa wizara, amesema hatua hio imefikiwa kuzuia kuenea ugonjwa wa aina yoyote wa kuku kuingia kwenye kuku wa nchini na kuzuia uingizaji holela wa vifaranga bila kupitia utaratibu na sheria zilizopo.

Amesema hasara ambayo ingeletwa na vifaranga 6400 kama wangeingia kwa namna waliyoingia na kuleta madhara yangekuwa makubwa zaidi kuliko yanayoonekana kwa kuteketeza vifaranga 6400.

Alipoulizwa kama hakukuwa na namna nyingine ya kuviaribu zaidi ya kuviteketeza hadharani, amesema havikuchomwa hadharani na amesema waliosambaza hizo picha walikuwa na lengo tofauti, amesema vitu vinavyofanyika nje ya hadhara maana yake havitakiwi kuonekana kwenye hadhara na mtu akikiuka ndio analeta madhara kama yaliyotokea.

Amesema utaratibu wa kuwachoma umetumika pia na mataifa mengine akitolea mfano Ulaya kilipotokea kichaa cha Ng'ombe lakini amesema sio kitendo cha kumuonyesha kila mtu ndivyo walivyofanyiwa.

Kuhusu kuwapima, amesema hawawezi kupima vifaranga ambavyo tangu awali walishatoa katazo visiingie nchini.

uchomaji moto sio kweli,unless watuambie kuwa walikuwa na magonjwa huu ni uongo ,kwa sasa kuna ugonjwa wa mafua ya ndege katika baadhi ya nchi za SADCC ila hawatumii njia ya kuchoma moto wale kuku walioathirika na ugonjwa huu,tatizo la viongozi wetu bado wanafikiria ni wao tuu wenye uwezo wa kupata habari.
 
Wizara ya mifugo na uvuvi imetetea uamuzi wa kuchoma vifaranga kwani ni utaratibu unaotambulika kimataifa na kwa mujibu wa sheria namba 17 wa sheria ya wanyama ya mwaka 2003 imechukua uamuzi huo wa kuteketeza vifaranga hivyo 6400 ili kuepusha kusambaza mafua ya ndege.

Kuhusu kuwapima, amesema hawawezi kupima vifaranga ambavyo tangu awali walishatoa katazo visiingie nchini.

Kumbe ni chuki baina ya viongozi wa nchi hizi ndo zinaingiza hasara kwa wananchi.
 
Serikali imeonya wanaosambaza picha za vifaranga kuchomwa moto na kusema hazifai kusambazwa kwani kitu hicho walikifanya sehemu ya siri ila ikatokea watu wasio waaminifu wakapiga picha na kuzisambaza

Akihojiwa na Azam Tv katibu mkuu wa wizara upande wa mifugo Dk. Maria Mashigo alisema wamevichoma moto kwa kuwa vingeweza kueneza magonjwa

Alipohojiwa kuwa wana ushahidi kuwa vina magonjwa kabla ya kuchoma moto alijibu hawakuwa na na haja ya kufanya hivyo

d5c3065e8e7d773a5acb54baf7a963d7.jpg
 
Picha zipo kwenye utube tayari nyie ndiyo mnakurupuka, hapo ni sawa na kuwaambia watu nendeni kwenye utube muone tunavyochoma vifaranga kutoka Kenya
 
Wizara iko sahihi ,Kuhusu bidhaa zisizo na ubora kama zimethibitika na mamlaka husika zinapigwa chini, mbona tunachoma vifaa fake vingi kutoka nje? ni mara ngapi vitu vimepatikana airport au bandari tena macontainer yanakamatwa na yanachomwa moto? je huwa tuna ugomvi na hizo nchi ambazo watanzania wamenunua bidhaa hizo? tatizo tumekubali kujenga undugu usio na tija na nchi jirani hivyo kupelekea kushindwa kusema hapana hata kwa mambo yasio na msingi, tukipata chickenpox ndo tutajua ni kwa nini serikali inakataza hao vifaranga.

Kikubwa ambacho kitaleta stability kati yetu na nchi zote za jirani, ni serikali ya Tanzania kuanza kutenga maeneo maalum kwa ajiri ya kuchungia mifugo hasa kwa wananchi wanaoishi maeno ya mipakani au karibu na mipakani.
 
Serikali imeonya wanaosambaza picha za vifaranga kuchomwa moto na kusema hazifai kusambazwa kwani kitu hicho walikifanya sehemu ya siri ila ikatokea watu wasio waaminifu wakapiga picha na kuzisambaza

Akihojiwa na Azam Tv katibu mkuu wa wizara upande wa mifugo Dk. Maria Mashigo alisema wamevichoma moto kwa kuwa vingeweza kueneza magonjwa

Alipohojiwa kuwa wana ushahidi kuwa vina magonjwa kabla ya kuchoma moto alijibu hawakuwa na na haja ya kufanya hivyo

Hapa kama ni kweli kwa kweli wamebugi, wangevirudisha huko huko.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom