Wizara muhimu zote zinaongozwa na Wanawake (Ulinzi, Afya, Elimu, TAMISEMI, Teknolojia, Foreign) sasa tunasubiri Jaji Kiongozi

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
10,018
2,000
Ni kweli kwa sasa Wanawake wanaweza wao wenyewe bila kuwezeshwa kwa sababu wizara zote wanazoongoza so far zinafanya vizuri.

Mulamula yuko vizuri, Ndalichako anasonga mbele, Ummy anatuvusha na Gwajima anazidi kutuimarisha.

Hata bungeni Dr Tulia anafanya vizuri sana pamoja na Katibu wa bunge.

Pale mahakamani ndio bado hapajabalance lakini tunategemea Rais Samia atapabalansisha kwenye uteuzi wa Jaji Kiongozi

Mungu ni mwema wakati wote!
Wanaume wengine bwana, kama wamechomwa ganzi vile!
 
Oct 27, 2020
97
400
Wote hao mpaka sasahivi wameunderperform. Elimu yetu bado kizungumkuti, Tamisemi hakueleweki, foreign affairs alisifiwa mwanzoni Ila nae hamna kitu. Hata hao wengine wapya pia wataunderperform.

Uanamke usiwe kigezo cha mtu kupata uongozi, bali uwezo. Ni vile Samia anataka kutumia karata ya wanawake kujizolea umaarufu.
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,590
2,000
Akimtoa anabandika mama mwingine,wanataka kumiliki Taasisi za Fedha ikiwemo Benki Kuu.
 
Mwamba 777

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
795
1,000
Ni kweli kwa sasa Wanawake wanaweza wao wenyewe bila kuwezeshwa kwa sababu wizara zote wanazoongoza so far zinafanya vizuri.

Mulamula yuko vizuri, Ndalichako anasonga mbele, Ummy anatuvusha na Gwajima anazidi kutuimarisha.

Hata bungeni Dr Tulia anafanya vizuri sana pamoja na Katibu wa bunge.

Pale mahakamani ndio bado hapajabalance lakini tunategemea Rais Samia atapabalansisha kwenye uteuzi wa Jaji Kiongozi

Mungu ni mwema wakati wote!
natamani na mkuu wa majeshi ateuliwe mwanamke,

na IGP wa police ateuliwe mwanamke

na waziri mkuu ateuliwe mwanamke

natamani nchi iwe ya kike.
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,796
2,000
Wote hao mpaka sasahivi wameunderperform. Elimu yetu bado kizungumkuti, Tamisemi hakueleweki, foreign affairs alisifiwa mwanzoni Ila nae hamna kitu. Hata hao wengine wapya pia wataunderperform.

Uanamke usiwe kigezo cha mtu kupata uongozi, bali uwezo. Ni vile Samia anataka kutumia karata ya wanawake kujizolea umaarufu.
Nyinyi wanaume mumetupelekesha wapi miaka yote hiyo? WAcha akina mama waongoze tuone mafanikio yao.

Ndiyo.... IGP, Mwanasheria Mkuu, Jaji kiongozi, CAG.... na wengine wengi wapewe nafasi wanawake zamu yao mara hii.

Muliona utendaji wa mama Anna Makinda kama Spika ulikuwa safi sana.....
 
Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,148
2,000
Tatizo ni kupiga dili!

Si ulimuona Jaffo alivyikuwa anarukaruka Tamisemi tukaamini anajenga madarasa kumbe hamna lolote usanii mtupu!
Usanii, usanii... Du CCM ni ile ile. Muigizaji ndio anayefahamika kwa lugha zao. Watanzania tunasafari ndefu.

Mmama alipomtoa TAMISEMI wengi tulishangaa, lakini tumemuelewa mama kuwa huyu kijana Jafo alikuwa mpigaji vile vile.
 
Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
758
1,000
Anayeunda serikali ni nani ujerumani?
Chansellor, ila ni kwa matakwa na nguvu za viongozi wengine(hajiamulii tu). Viongozi hao ni pamoja na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.

Kifupi nchi hawezi kuiongoza yeye kama yeye pasipo msaada wa wanaume wa shoka pembeni. Chukulia England.
 
RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,279
2,000
Hata wajaze wanawake wote lakini katibu mkuu kiongozi akiwa Mwanaume mambo poa tu!!Huyo ndio mboni ya Raisi awapo madarakani!!!
 
Sentebe

Senior Member
Jul 12, 2014
185
250
Pale IGP afande Kaganda anafiti kinoma, l Mama tufanyie mchakato CDF na TISS boss wawe kinamama, tunahitaji mapinduzi ya kweli ya kuendeleza nchi, na nchi hii ili iendelee akina Mama wawe mbele kwenye nyanja zote za uongozi na mihimili yote.
Wana mshakanywa na mama mtulize vitenesi msije dundishwa.
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,587
2,000
Swali la maana ni kama wanaweza na sio ni jinsia gani....

Haya mambo ya 50 / 50 ni upuuzi uliokithiri..., Ubaguzi / Upendeleo ni Ubaguzi tu..., iwe ni Rangi, Jinsia, Kabila au Chochote kile..., kwenye utendaji inabidi kuwa na Ubaguzi wa aina moja tu..., nao ni UWEZO
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom