Wizara inayotakiwa kufanyiwa mabadiliko makubwa ni Afya

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,634
7,010
Namkubali Ummy Mwalimu kabisa,lakini,mkitaka kuiokoa wizara hii, vigogo wengi wanatakiwa kung'olewa hapo kwani wamekuwa chanzo cha matatizo mengi makubwa.mf. ni kitengo cha mafunzo.

Wanaweka taratibu za ajabu na imesababisha hadi sasa wameshindwa kutoa matokeo ya mitihani ya mwaka jana.

Wizara ya elimu inasahihisha maelfu ya wanafunzi na inatoa matokeo kwa muda muafaka,sasa kwa nini wasiachiwe NACTE kufanya kazi hiyo?Kuna watu pale hawajali kabisa maisha ya watu.

Kama yasipofanyika mabadiliko makubwa hapo, mambo yatazidi kuwa mabaya. Kuna watu bado wanafanya kazi kwa mazoea na viburi vya madaktari
 
Sio wizara ya afya tu kote serikalini viti vimekaliwa na wazee wenye fikra za miaka ya 80..ni baba zetu kweli Lakini uwezo Wao mdogo Sana watendaji wengi wa serikali wameshachoka(ga).. Cha msingi ambacho rais angekifanya na nchi ikaenda Kwa KASI Sana ni hivi.. Kuanzia wale Wakuu wa vyombo vya usalama wangepigwa chini NAFASI hizo wapewe vijana.. Kwenye maofisi ya serikali toka zamani mtu amekalia cheo KIMOJA. Me Nashangaa Sana hii nchi yaani NAFASI za kiutendaji zinaendeshwa kisiasa.. MFANO mahali pangu Ile management board ukiwaangalia wote wamechoka ni wazee Sana Sasa unajiuliza hivi kweli wana uwezo wa kujiongeza au VIPI.. Rais akitaka nchi isonge hata ndani ya miaka miwili tu. Awape vijana NAFASI hata vile vyeo vikubwa kwenye NAFASI za Ofis. Ajaribu tu hata Kwa mwaka aone. Mtu kashika ofisi toka Zama hawezi kujiongeza. Asiwafukuze kazi bali awashushe vyeo wawe wafanyakazi wa kawaida atafanikiwa Sana
 
Kwa hiyo hata rais naye ajipige chini maana naye si wa miaka ya sasa? Katibu mkuu kiongozi, jaji mkuu na orodha inaendelea. Nadhani ungeiweka vizuri zaidi kwa mfano useme, wazee wote wasio na mipango kazi ya dunia ya sasa, waachishwe kazi. Maana kuna wazee wanaofaa hata sasa, na si kila kijana ataweza kuwa na ufanyaji kazi unaoufikira kichwani, kuna vijana mawazo yao yatapitwa mbali na hao unaowaita wazee wa mawazo ya miaka ya 80.
 
kweli kabisa wizara ya afya ndo inaongoza kwa wapigaji,,mfano kuna watu kibao tu tulikua tunasoma nao medicine ila wakadisco wengine wakiwa mwaka wa kwanza lakini cha ajabu sasa hivi wana vyeti na wako mahospitalini ila sisi tulio faulu tupo mtaani na hatuna ajira,hii ni hatari sana kuona watanzania wenzetu wanatibiwa na mafelia..
 
Namkubali Ummy Mwalimu kabisa,lakini,mkitaka kuiokoa wizara hii, vigogo wengi wanatakiwa kung'olewa hapo kwani wamekuwa chanzo cha matatizo mengi makubwa.mf. ni kitengo cha mafunzo.

Wanaweka taratibu za ajabu na imesababisha hadi sasa wameshindwa kutoa matokeo ya mitihani ya mwaka jana.

Wizara ya elimu inasahihisha maelfu ya wanafunzi na inatoa matokeo kwa muda muafaka,sasa kwa nini wasiachiwe NACTE kufanya kazi hiyo?Kuna watu pale hawajali kabisa maisha ya watu.

Kama yasipofanyika mabadiliko makubwa hapo, mambo yatazidi kuwa mabaya. Kuna watu bado wanafanya kazi kwa mazoea na viburi vya madaktari
Taratibu gani hizo mkuu kibaravumba ? Sio wote tunajua kinachoendelea huko
 
Hawa watu wanatakiwa kuchunguzwa na wachukuliwe hatua kwa uzembe,ubinafsi,kiburi na umungu mtu.Hawajali wala kuogopa mtu yoyote
 
Taratibu gani hizo mkuu kibaravumba ? Sio wote tunajua kinachoendelea huko
Ni maelezo marefu mkuu ila kwa walengwa wanajua jinsi wizara hii inavyowaumiza kiuchumi,kisaikolojia na kiakili.Ni wizara yenye mipango mibovu na wanaopanga mipango hiyo Hawajali hata kama ina athari kwa wengi.Wao wanachoangalia ni maslahi yao pekee.Napendekeza wakurugenzi wote wang'olewe na umakini wa kuteua uwepo.
 
Sio afya tu Mkuu kuna MAMA NDALICHAKO,,
Anatesa sana RAIA utafikili atakuwa wazili miaka 1000 yan
[HASHTAG]#Elimu[/HASHTAG] ya matamko Leo hili kesho lilr
##Twafa
 
Tatizo kuu la wizara ya Afya kwa sasa ni Ummy Mwalimu. Ni waziri wa ovyo kabisa anayeendesha wizara nzito kwa kutumia Twitter, instagram, Facebook nk.

Sijawahi kuona waziri wa ovyo kabisa kama Ummy Mwalimu aliyewahi kupewa wizara ya Afya toka tupate uhuru. Ummy anajua kuimba Propaganda tu, anadhani wizara ya Afya ni jukwaa la kufanyia siasa za kuunga unga ili kumpendezesha rais. Hajui kuwa wizara ya Afya ni maisha ya watanzania.
Hajui chochote kuhusu utaalamu wa Afya lakini anawapelekesha ovyo ovyo wataalamu wa hali ya juu katika wizara ile.

Bahati mbaya sana Naibu waziri wa Afya(Dr.Hamisi Kigwangwalla) ni kiumbe mnafiki, mwoga na Mfitini sana. Hana msaada wowote pale.

Mtu pekee pale wizara ya Afya mwenye kujitambua na kujielewa ni Katibu Mkuu (Dr.Mpoki), lakini kwa bahati mbaya sana hana mamlaka ya kimaamuzi.
Ningekuwa mimi ndio Dr.Mpoki ningeachia ngazi mapema sana na kwenda kufanya kazi zingine kuliko kubakia kupelekeshwa kama karani kwenye duka la Mhindi bahili.
 
kote matatizo yapo inchi nenda mahakamani hasa za mwanzo ,makarani wanaajiriwa kwa vigezo gani? wengi ni wale jamaa au ndugu wa mahakimu na darasa la saba.karne hii.
 
kweli kabisa wizara ya afya ndo inaongoza kwa wapigaji,,mfano kuna watu kibao tu tulikua tunasoma nao medicine ila wakadisco wengine wakiwa mwaka wa kwanza lakini cha ajabu sasa hivi wana vyeti na wako mahospitalini ila sisi tulio faulu tupo mtaani na hatuna ajira,hii ni hatari sana kuona watanzania wenzetu wanatibiwa na mafelia..
Kashfa nzito hii, hebu weka ushahidi
 
Back
Top Bottom