Wizara Hizi Zifutwe Haraka!

K-Boko

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
697
195
Mbunge wa Mtera (CCM) Mh. Livingstone Lusinde ameishutumu serikali kwa kutoweka umuhimu kwa Wizara kadhaa ikiwemo Afya na Maendeleo ya Jamii na akakejeli kuwa ni afadhali wizara hizo zifutiliwe kwa mbali! Ameendelea kudai mawaziri wa Tanzania hawana seriousness. Akadai inakuwaje waziri anaingia Facebook wakati wa mijadala ya Bunge? Yaani jamaa kakandia mbaya! Akataka yatengenezwe mazingira kwa watoto wa masikini (kama yeye) kuweza kupenya katika mizengwe ya mazingira ya sasa ya nchi na kuendelea kimaisha. Pia ametaka wabunge wawe serious kuwaondoa mawaziri waliotajwa kuwa wachovu na wabovu badala ya kuwachekeachekea! Siku za hivi karibuni mawaziri kadhaa akiwemo PM Pinda na Hawa Ghasia wametuhumiwa kuwa wabovu na wametakiwa kuachia ngazi!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom