Wivu wa mapenzi wasababisha majeraha!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wivu wa mapenzi wasababisha majeraha!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by futikamba, Apr 26, 2010.

 1. futikamba

  futikamba JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2010
  Joined: Jan 18, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hi Wana JF,
  Nna mpenzi wangu ambaye tupo wote kwa miezi 7. Tunapendana sana. Tatizo ni moja,hatuishi kugomanbana na kupigwa jamani. Yaani tukigombana kidogo tu, mwanzangu anatumia ubabe kunipiga. Na hili linatokana na wivu alionao mpenzi wangu. Ana wivu kupita kiasi, wivu huu unasababisha hadi shughuli za kimaendeleo zinadoda. Juzi tumegombana sana mpaka kupigana. Kisa, ni kama wiki tatu zilizopita, nilifuma message za wanawake 5 tofauti kwenye simu yake wote wakiwa wapenzi wake. Nikagombana nae sana mpaka kuachana. Ila tulikuja tukapatana kama baada ya wiki na nusu hivi since aliniomba sana tusiachane. Anayway, nikamkubalia. Sasa, siku moja akapekua simu yangu akakuta nimeandikiwa message na bosi wangu kwamba nikipata muda nimtafute. Sio personal!! Yeye akamtukana kweli-kwa simu na sms. Mi siku hiyo sikutaka ugomvi, nikanyamaza tu lakini nilikuwa naumia kweli kwa ndani. Sasa juzi tukakorofishana kitu kidogo mi nikamuuliza kwanini alimtukana boss wangu? And anaelewa kabisa huyo ni boss, nikikosa kazi atanisaidiaje?? Na kusema kweli hanisaidii hata shopping ya kula tu. Yaani yeye gharama yake ni pale anapohitaji kunanilii nd'o pesa itamtoka. Alikuja kwangu juzi usiku kanikuta nimelala, akaanza kunigombeza na kunipiga. Kweli nilipandwa na hasira, nikampiga na chupa ya kichwani. Ameshonwa nyuzi za kutosha. Sijawahi kufanya kitendo hicho maisha yangu yote, hii imetokana na hasira na najutia kweli. Huyu mpenzi ananifaa kweli? Yaani, sijaelezea yote.... ningejaza kurasa tatu hapa ila kwa kifupi nipo kwenye stress ya hali ya juu. Mi mwenyewe nna nundu kichwani. Yeye ana donda. Inaniuma kumpiga kiasi hicho, lakini yeye nd'o anasababisha kila siku tunagombana kwa sababu ya wivu wa vitu vidogo vidogo tu. Nipeni ushauri watu wenye busara.....
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  shosti kimbia usigeuke nyuma...huyu kabla hajakutoa roho kwa kipigo atakuuwa kwa magonjwa....kwa ufupi ni kwamba huyu hana mapenzi ya kweli anakutumia tu...mama chapa mwendo achana na kimeo hicho...
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nyie wote "you dont match one-another"!...Inafikia wakati kwamba lazima ukweli uwekwe hadharani, regardless ya mapenzi ya kutamaniana mliyo nayo!

  Hakuna mapenzi hapo ati!

  Nawashauri mapema kila mtu atafute mtu ambaye anaweza kuishi nae kwa amani, badala ya kupotezeana muda!

  Wewe mdada nae pia una roho ngumu/mbaya sana, kweli unathubutu kumpiga CHUPA mwanaume kichwani?..mi ni mwanaume lakini sijawahi kuota jambo hilo maishani!...Una hasira kali sana, ambayo ni hatari sana kwa kiumbe anayeitwa mwanamke...utakuja ua mtoto ati!!

  Hata ukija kupata mtu mwingine uangalie sana, maana bila kujirekebisha usitegemee jipya!..

  Nimemaliza!
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hapana....alikuwa anajihami baada ya kugeuzwa ngoma kila siku anapigwa....mbona hujasema huyo jamaa anayempiga nae ana roho mbaya kama ziraili?
   
 5. b

  bwanashamba Senior Member

  #5
  Apr 26, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DADA la kwanza uyo bwana siyo ata kidogo matumizi atoi
  mpaka atake kamchezoooooo lo uyo bwana mangi nini'ila take care uyo
  bwana hana mapenzi ya kweli ata kidogo na yeye ana tabia mbaya ndo maana
  anakuisi wewe na kuzidisha kawivu'
  nawewe pia ulifanya makosa kumpiga mwanaume na chupa ;je ingekua jamaa mkurya
  si kuna siku ungemchoma na kisu kabisa JIREKEBISHE USITUMIE SILAA
  KUMPIGA MWANAUME'
   
 6. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2010
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Preta umesahau ule usemi "mkuki kwa........................................."

   
 7. 1

  1985 New Member

  #7
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 26, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mshukuru Mungu kwa kukuonyesha hayo kabla ya kuingia kwenye mkataba wa ndoa, kimbia sana maisha yenyewe mafupi asije kutoa roho bure
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Bwanashamba..
  Una point kali sana, nimekugongea THANKS.
  Ila shida moja, color uliyotumia inaua macho aisee!...wenzio hii ndo ofisi ati!
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  run my dear ...run! run vevry fast wala usitizame nyuma! duh

  hakupendi huyo anakutumia tu. angekupenda singekuwa na wanawake watano! angekupenda asingemtukana bossi wako. angekupenda asingejaribu kukupiga licha ya kukupa nundu! ......

  mkimbie na akikuganda sana peleka polisi
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mdada, huyo hakufai na angalia kidogo kidogo anakufanya wewe uwe mkatili... kitendo cha wewe kumrushia chupa kinaonyesha umeanza kuwa kama yeye, yaani mkatili, tusubiri uwe mzinzi na uharibike kabisa

  CHAPA MWENDO
   
 11. m

  masho Member

  #11
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dada kimbia kadri uwezavyo katili huyo, mapenzi ya kupgana nani anayataka, ataja kutoa roho hulo na magonjwa ya ajabu
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Apr 26, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Dada pole sana

  Dada nadhani hapo inabidi utoke.Kama

  jama ana mademu watano tofauti,

  Anamtukana boss wako huku akiwa hana uhakika kama unatoka na bosi

  Hana Moyo wa kukusaidia unapohitaji msaasada hata wa chakula,achilia mbali kukupa sapoti ukiwa huna kazi

  Ugomvi wake unapelekea kupigwa

  Sidhani kama hapo kuna mapenzi ya dhati.inawezekana kabisa wewe unampenda jamaa lakini sidhani kama yeye ana mapenzi.Zama za kupiga wanawake zimepita.Pia kitendo cha jamaa kutoa tu matusi kwa bosi wako bila uhakika kinaonyesha jama hana ustaarabu wa maisha na wala mapenzi

  Dada jaribu tu kuachana nae.Ni miezi saba tu?sidhani kama huyo jamaa mtafikishana nae sehemu salama

  Pia na wewe usiwe na kiburi unapoulizwa ishu yoyote uwe unatoa majibu ya kistaarabu coz inawezekana kwa vile ulipata sms za madem wengine basi na yeye akikuuliza sms za majamaa wengine unajibu kwa nyodo na kukmkumbushia msg ulizokuta kwenye simu yake siku zilizopita huku mkiwa mmesha-solve hizo issue.

  Pia kitendo cha kumpiga na chupa hakikuwa kizuri,ungeweza kusababisha kifo na kuingia kwenye kesi ya jinai pamoja na dhambi ya mauti dada. Kwa ajili ya heri ya baadae ni bora tu utafute mchumba mwingine(usiwe player lakini),uanze maisha upya.Mungu akutie nguvu dada
   
 13. joellincoln

  joellincoln Senior Member

  #13
  Apr 26, 2010
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole dada ila kusema ukweli huyo jamaa hakufai wewe cha kufanya funga ukurasa wa zamani na anza maisha mapya utapata tu mtu anayekufaa kuliko kuishi na endoparasite ambaye hakujali na focus yake ni ile TAMUUUU tu, otherwise ni ugomvi. Na hii ni indication huyo mwanaume si mwaminifu na ndo maaana ni mgomvi na ana wivu wa kupindukia hizi ni dalili kuwa mko wengi sanaa, so anapokuja kwako anahisi yale anayoyafanya yeye na wewe unayafanya ndo maana anafikia hatua ya kumtukana mpaka boss wako. Hakutakii mema huyo. Kimbia mapema wala usigeuke nyuma dada! Ila punguza au acha kabisa matumizi ya silaha unapojihami, maana unaweza kuuua bila kukusudia na mahakama zetu hizi mpaka waje wajue hilo mama utakuwa umekula mvua za kutosha huko gerezani.
   
 14. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ninyi wote wawili mna matatizo makubwa tu. Hampendani, ila mnatumiana tu kwa sababu ya tamaa. Hajatulia wote. Achaneni mapema kabla hamjatoana roho kwani huko ndiko mnakoelekea msipoachana. Leo wewe una nundu kichwani mwenzako ana ngeo. Kesho mtapiga hatua zaidi: nayo ni kumwaga damu ya mmoja wenu. Please wahini mapema kuachana.
   
 15. k

  kero Member

  #15
  Apr 26, 2010
  Joined: Sep 23, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe Dada unatamaa......
  Huyo mshikaji haumpendi ila hautaki kumuavha kisha alishaa kuduuu sana, na unaogopa jamaa siku akitoka, kwasababu huyo jamaa yako inavyoonekana ni mpiganaji na bado hajatoka, ila kwasababu we unaendeshwa na njaa unathamini boss, yeye sio mjinga kumtukana boss ni lazima boss alishakuaproach kuna jambo umetuficha wa JF, wewe ni kimeo tena kibaya in short you are material lady.
  Pia unabahati jamaa huwa anatoa pesa hata wakati anataka kudoo na wewe, wewe ka pesa unayo ya kula unahitaji upewe ya nini avha ulimbukeni wa kushobokea wanaume utaishia kuwa malaya, JF isikupoteze muombe msamaha mshikaji wako then kubali kunanihii bila vikwazo kwasababu pia hasira za mshikaji ni kwasababu haumpi freshi, inaonekana anakulazimisha kudoo always, Mademu wa type yako huwa mnaishia kuwa malaya na kuuwa wanaumezenu na kununua Vimario...
  Ofwhich ukiendekeza mwisho ni ukimwi tuu..
  Tabia inabadilika, muheshimu mshikaji wako utafanikiwa acha ushamba.
   
 16. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Futi kamba, kwamba wewe una Nundu na mjamaa ana lingeu. Huenda mmoja wenu atakuwa anatokea Tarime si bure. Hata kama anakubonda lakini mpaka mtoto wa kike umeweza kunyanyua chupa na kumchapa nayo basi umeshakomaa vya kutosha. Mimi natofautiana na wengine. Nadhani kwa hatua mliyofikia na huyo jamaa wala msiachane muendelee tu mpaka pale nyie wenyewe akili zitakapowarudia na kuona mnayofanya sio sawa then maisha yataendelea na mengine yatakuwa ni history tu. Kinachonifanya nikushauri hivyo ni kuwa kwa maelezo yako tayari mtoto wa kike umeshakuwa nunda na mkatili kiasi kwamba lazima akili na mwili wako vimeshaozoea kichapo, sasa hata ukija kupata mtu mtaratibu na muelewa hutowezana naye na hasa utakapokuja kugundua may be jamaa anadokoa kwa jirani ni wazi utamvuruga sana. Huyo Jamaa anakufaa sana kwa hatua mliyofikia....mzoea vya kunyonga vya kuchinja hawezi kamwe!!
   
 17. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,026
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Hivi Futi Kamba hii ni hoja ya kuileta jukwaani ilhali iko wazi kabisa. HAKUNA MAPENZI ni kuwaka tamaa tu mlikonako.
   
 18. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwa maongezi yooote hapa, inaonyesha wewe haujaolewa, utaishije na mtu wakati haujafunga ndoa? unazini dada, Mungu anakuona, hauoni aibu Mungu anakuona hata hivi unavyosoma meseji na anakutaka uache uzinzi. Waasherati na wazinzi hawataurithi uzima wa milele. ukiwa mzinzi, shetani anaweza akawachezea apendavyo, atawagongesha vichwa mtatoka manundu kila siku mnapondana, njoo kwa Yesu utapata mwanaume wa kutoka kwa Mungu, asiye mzinzi kwenye ulimwengu huu uliojaa ukimwi. kwanza umepima? kama ana wanawake wengine wengi hivyo, vipi unafikiri utaishi muda mrefu kiasi gani kama hautakuwa makini?

  I DON'TMEAN KUKUUMIZA, ila nakupa ushauri wa bure. shetani anaenda kuchochea kwa uyo jamaa yako, halafu anarudi kuchochea na kwako pia, halafu mkianza kuzipiga yeye shetani anakaa pembeni anachekelea, anawagongesha vichwa nyinyi kwa nyinyi, atawachezea hadi mchoke, mwisho atawaletea ukimwi, utakufa na utaenda jehanum. Nakushauri okoka leo, achana na kuishi na wanaume ovyo, tafuta mmoja, funga naye ndoa, vumiliana naye katika shida na raha, akikupiga mwombee, ataacha tu .....namaanisha huyo atakayekuwa kwenye ndoa. si huyo ambaye bado anatafutatafuta wa kukulinganisha ili akipata mtamu zaidi akupige chini. kalagabaho.
   
 19. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mhhh mie naona anastahili hiyo chupa kichwani... wala usione vibaya... Ondoka atakuumiza bure na anakufupishia maisha yako..utapata mwengine atakae kutreat better...
   
 20. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa mtazamo wangu, you don't match completely na wote mna matatizo makubwa. Kujirahisi kwako kumekuponza na ni heri uishie hapo ulipofika maana ukienedlea kuwa na moyo wa mama huruma yatakukuta makubwa.
  Take care
   
Loading...