Wivu wa design hii katika mapenzi ni hasara tupu.

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Mkazi wa Vingunguti Sokoine Mtunda, ameuawa na wananchi wenye hasira kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Faustine Shilogile, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 3:00 usiku huko Vingunguti kwa wachinja nyama.

Akielezea sababu ya kifo hicho, Kamanda Shilogile amesema, mtu huyo ambaye pia ni mchinjaji wa wanyama katika eneo hilo, anadaiwa kuwa usiku alirejea nyumbani toka mzigoni na kumkuta mkewe, Bi. Muta Mazengo, 25, akiwa na doti mbili za khanga mpya ambazo hazifahamu.

Alisema kutokana na hilo, Bw. Mtunda alimhoji mkewe alikozitoa khanga hizo kwa sababu anafahamu wazi kuwa mkewe hana uwezo wa kuzipata khanga hizo bila ya kununuliwa.

Amesema kutokana na kubanwa na maswali ya mumewe, mkewe alimtaja kijana aliyetambulika kwa jina la Bw. Hossen kuwa ndiye aliyempa khanga hizo.

Akasema kwa hasira mumewe alimbeba mkewe hadi kwa kijana huyo usiku ili kwenda kujua kulikoni hadi akampa mkewe kanga hizo.

Alisema Hussein alikanusha kuwa si yeye aliyempa kanga hizo, ndipo alipomuitia mwizi Bw. Mtunda,ambapo wananchi wenye hasira walijitokeza na kuanza kumshambulia kwa fimbo na vitu mbalimbali hadi kumuua.
 
yakhe mie sijaona kosa la marehemu,we ulitaka akae kimya?yakhe ilibidi kile kichwa cha habari ungebadili.Mie naona marehemu ajafanya kosa,hivi kama unamuachia mkeo mia tano(si kama unapenda ila ni hali ngumu ya maisha)then ukirudi toka mianjo yako unakuta wali kuku au pilau,vipi utakula au ?kumbuka mkeo hana kipato chochote
 
Interesting!

...fidel80, Situation hiyo kwa mfano; wewe ndio 'Sokoine mtunda', unge react vipi na kuchukua hatua gani baada ya 'mkeo' kukwambia 'Hossen' ndio alokupa 'khanga'!?
 
hala hala kirobot maana nahisi ungeweza ku mudhihir mudhihir bin kumchinga sound mbaya wako!!
 
Sioni kosa la marehemu, ila imeonyesha nini umuhimu wa kumwelewa mwenzio na udhaifu wake, iwe mke au mume. Kama jamaa angejua fika udhaifu wa mkewe tangu awali huenda asingemuoa. Lakini, NO huenda mke ni muaminifu mno kiasi hakujua hata jinsi ya kuficha uzinzi aliouanza. Kwa watoto wa mjini haswa sidhani hilo lingetokea.
Nimemsikitikia alivyopoteza maisha. Somo kwetu wengine.
 
tatizo la marehemu lilikuwa mkono mfupi kwa mkewe alikuwa anyoshi mkono ndo maana Hossen akampata kilaini na kuamua kugharamia faster.........
 
Mbaya kabisa masikini mke kamuua mumewe bila kukusudia! damn
 
Wivu ndio wenyewe ila usizidi ila mwanamama ndiye mwenye makosa 100percent na ametenda zambi kubwa sana,ila inauuuumaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Labda huyo mama alitaka mumewe azione hizo kanga. Kama anajua mumewe ana wivu, kwanini hakuzificha?
 
tatizo la marehemu lilikuwa mkono mfupi kwa mkewe alikuwa anyoshi mkono ndo maana Hossen akampata kilaini na kuamua kugharamia faster.........


Acha hizo fidel siyo mkono mfupi, labda hakuwa na pesa.
si unajua maisha magumu
 
Mi naona ishu hapa ni huyu mjingamjinga aliyeamua kumwitia mwenziwe mwizi, na huku akiwa na kosa la pili la kuiba mke wa mtu!

Ni mtu mbaya sana huyu, na ameonyesha kweli kabisa kuwa alikuwa ni mharibifu wa nyumba ya watu ndo maana reaction yake ikawa ya kuita wauaji ili kuua ushahidi!
 
Inasikitisha sana hali hii,huyo hossen amefanya dhambi,marehemu kafa akitetea haki yake ya msingi kwa mkewe(kama alioa kihalali kwa mujibu wa imani)
 
Mie namlaumu huyo mwanamke, kama kweli ni mwaminifu kiasi hicho mpaka kumtaja aliempa hizo kanga, basi hakuwa na haja ya kuzipokea. Nadhani alikuwa na mpango wa kumuua mumewe na huyo jamaa yake.
 
Back
Top Bottom